Dr. Nicole Cross-Camp
ambaye ni Mtafiti kutoka Chuo kikuu cha East Anglia cha nchini Uingereza chini
ya mradi wa ESPA (Ecosystem Services for Poverty Alleviation) akitoa
mada kuhusiana na matokeo ya utafiti kuhusu changamoto wanazozipata
wanakijiji katika utunzaji wa misitu kwa wadau kutoka Wizara mbalimbali pamoja
na Sekta binafsi.
Maneja Mradi, Lasima
Nzao akiwasilisha matokeo ya utafiti uliopo chini ya mradi wa ESPA
(Ecosystem Services for Poverty Alleviation). Mkutano huo ulifanyika
katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Wadau
wa Mistu na Mazingira kutoka Serikalini, Taasisi na Mashirika binafsi walikutana
na watafiti hao ili kujadili matokeo hayo ya utafiti na kuweza kuchanganua
mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na changamoto na faida zinazotokana na
usimamizi wa misitu kwa wanajamii wanazozungukwa na hifadi ya misitu hapa
Tanzania.
Akizungumza
na Lasima Nzao na Dr Nicole Gross-Camp walisema kuwa utafiti
huo uliofanyika katika vijiji nane vya wilaya mbili, halmashauri ya wilaya
ya Iringa vijijini na wilaya ya Kilwa kuanzia Septemba 2014 na kumalizika
september 2016 na ulikuwa "unaangalia mchango wa misitu inayosimamiwa na
Jamii (CBFM) katika kuboresha hali ya maisha kwa wanakijiji
husika".
Utafiti
unaonyesha kuwa mistu na mazingira ikisimamiwa ipasavyo inaweza
kuboresha maisha ya wananchi walio vijijini kwa kuwa wanajamii wanapenda mfumo
wa misitu ya jamii japokua bado kuna changamoto nyingi katika usimamizi wa
misitu kwa wanajamii hasa misitu inayosimamiwa na Jamii.
Utafiti
huo ulidhaminiwa na ESPA, UKAID, NERC na ESRC na ulifanywa na mtafiti kutoka
Chuo Kikuu cha East Anglia UEA nchini Uingereza Dr Nicole Gross-Camp
akishirikiana na mtafiti kijana wa kitanzania, Lasima Nzao ambaye pia alikua
meneja wa mradi wa Utafiti huo.
Mtafiti
na Mshauri wa masuala ya Misitu, Kihana Lukumbuzya akichangia mada
baada ya wataalamu kuwasilisha utafiti uliofanyika katika vijiji nane
ndani ya wilaya mbili.
Mshauri
wa masuala ya Misitu na Mabadiliko ya Tabianchi, Faustine Ninga
akichangia mada kuhusu utafiti uliofanyika katika wilaya mbili kuhusu
mchango wa jamii (CBFM) katika kuboresha hali ya maishaya wanajamii.
Gabriel Marite Ole Tuke
Msimamizi wa Maliasili kutoka Mkoani Dodoma, Sanford Kway akichangia mada
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment