Thursday, September 15, 2016

UVCCM YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU VURUGU ZA JIJINI ARUSHA,YAMSIMAMISHA KAZI KATIBU WA UVCCM ARUSHA


Jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM imemsimamisha kazi aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ezekiel Mollel kwa kutotiii agizo la Makao Makuu linalomtaka kuhama na kusibabisha mvutamo na malumbano yasio na tija kwa chama cha Mapinduzi mkoani Arusha.

Pia Jumuiya imewataka vijana wa uvccm kutambua kuwa shughuli za uendeshaji wa umoja huo zinafanyika kwa kufuata taratibu za kikanuni chini ya misingi ya nidhamu na utii.

Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka Hamdu Shaka amewaeleza wandishi wa habari katika ofisi za UVCCM mkoa wa Arusha mara baada ya kumaliza mzozo ulioibuka na kusababisha baadhi ya vijana kufunga ofisi wakimkataa Ezekiel asiendelee kubakia mkoani hapo.

Shaka alisema tokea tarehe 25 August makao makuu ilimuandikia barua Mollel kumuhamishia Makao Makuu Dar Es Salam lakini cha ajabu kwa muda wote amekuwa akikaidi kuhama kwa sababu zake binafsi.

Alisema kikao cha sekreterieti ya Taifa kilichoketi jijijini Dar es salaam 14 September kimeamua kumsimamisha kazi katibu huyo na kumtaka ampishe katibu wa mkoa mpya Said Goha aliyehamia Arusha akitokea lindi

"Mollel amekuwa akidai kuwa Arusha kuna harufu ya ubadhirifu wa mali na miradi ya Jumuiya, Makao makuu haijapinga dai hilo , kuhama kwake si kikwazo cha kuzuia kubaini nani amehusika na tuhuma hizo, amehamishwa kwa sababu za kawaida pia kutokana na sintofahamu iliopo "alisema shaka.

Alipoulizwa iwapo ni mpango wa kukuondoa ili kuficha ukweli wa ufujaji wa miradi alisema kuhama kwake hakuwezi kuzuia ukweli usijukikane, kwani Jumuiya inafanya uchunguzi wa miradi na rasilimali zake pia vyombo vya serikali vimeombwa viingiliie sakata hilo ili kupata ukweli wa mambo.

"Mtumishi unapohamishwa toka kituo kimoja kwenda kingine na kukataa huo ni uvunjaji wa taratibu, ukiukaji wa kanuni na kutoonyesha nidhamu ya kazi, amesimamishwa kazi hadi jambo lake litakapifikishwa katika vikao vya kitaifa vyenye mamlaka ya uteuzi wake wa mwisho kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM"alieleza shaka

Akijibu swali la mwandishi kwamba katibu huyo amekuwa akikaidi kuondoka kwa sababu analindwa na baadhi ya wakubwa wa makao Makuu pia makao makuu ikitaka kumlinda kiongozi mmoja wa juu asihusishwe na ubadhirifu huo, shaka alikana na kusema wanaoeneza maneno hayo ni mashabiki wa kisiasa..

"Nasema vijana wenzetu wa Arusha wafahamu uendeshaji wa kazi zetu ni uzingatiaji wa taratibu na kikaanuni, makao makuu haiwezi kumkingia kifua mwizi na kumtetea , kumlinda na kumtetea mvunja taratibu husika "alisema.

Aidha Kaimu huyo Katibu mkuu alisema kazi ya ufuatiliaji miradi, mikataba , mapato na matumizi yake yatafuatiliwa hatua kwa hatua na ukweli wa jambo hilo utaanikwaa bila mtu kulindwa na kuogopwa.

Hata hivyo shaka alipoulizwa kwamba makao makuu imeshindwa kumchukulia hatua za kinidhamu mwenyeikiti wa mkoa huo Lengi Sabaya anayedaiwa kufanya hadaa na kukutwa na vitambulisho feki , alijibu kuwa madai hayo ni binafsi yenye mwekeleo wa jinai na iwapo kweli anakabiliwa na tuhuma hizo vyombo vya dola vipo na vinapaswa kuchukua hatua haraka UVCCM haitamlinda mtu katika jambo lolote lililo kinyume na maadili ya Chama.

Pia akiwataka wana Jumuiya kuacha tabia ya kubuni au kubashiri mambo ambayo mtu hana ushahidi nayo akidai kwamba kiongozi fulani anamlinda mtu fulani wakati hakuna kiongozi makini anayeweza kumlinda mtu anayekiuka kanuni na kuvunja taratibu halali

"chama chetu kina Katiba jumuiya yetu ina kanuni toleo la 2012 tuna kanuni ya utumishi kanuni ya fedha na maadili iyo ndio miongozo yetu katika kutekeleza majukumu ya kila siku hatutafumbia macho mtu yoyote atakaepindisha mstari mmoja wa kanuni au taratibu kwa vile hakuna aliye juu ya miongozo hiyo" alisema shaka

Amewataka vijana wa Arusha kuwa watulivu kwani viongozi wote wako makini katika kila jambo na jumuiya Arusha itaendelea kubaki salama.

Shaka amewasili mkoani arusha jana kufuatia kuibuka kwa mzozo uliosabanisha baadhi ya vijana kumfungia ofisi katibu aliyehamishwa Ezekiel molel ambae anaungwa mkono na Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa huo kwa madai amempa kazi afanye na hajakamilisha.

No comments: