Wednesday, September 14, 2016

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Baadhiya wabunge wakiingia katika ukumbi wa Bunge kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoendeleo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Mwigulu Nchemba akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mijadala bungeni leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma ambapo alisema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili (2) katika mfuko wa mazingira kwa ajili ya zoezi ya upandaji miti ili kutunza mazingira.
Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma ambapo alisema kuwa agizo la Rais Dkt. Magufuli la kuhakikisha viwanda vinavyobinafsishwa vinafanya kazi linaendelea kutekelezwa tangu Novemba 2015.
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Azzan Musa Zungu akiendesha kikao cha bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba akiwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

No comments: