Wednesday, September 14, 2016

Tamasha la uhondo wa Zantel lakongo nyoyo za wakazi wa Tameke

 Msanii wa muziki wa bongo flava, Seif Mwinjuma ‘sholo mwamba’ akiimba
katika tamasha la Uhondo wa Zantel lililofanyika katika viwanja vya
Temeke Mwisho, Dar es Salaam hivi karibuni ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu ya mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma mpya zilizopo sokoni.
 Meneja Habari na Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Zantel, Winnes Lyaro
(kulia), akitoa maelezo kwa baadhi ya wakazi wa Temeke, Dar es Salaam
 kuhusu huduma na bidhaa  mpya zitolewazo na kampuni hiyo wakati
wa tamasha lililopewa jina la ‘uhondo wa Zantel’ lililodhaminiwa na
kampuni hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ally Momba ‘Momba’ akionyesha umahiri
wake wa kuimba katika tamasha la Uhondo wa Zantel lililofanyika katika
viwanja vya Temeke Mwisho, Dar es Salaam ikiwa ni moja ya kampeni
za kampuni ya simu ya mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake
ikiwajulisha bidhaa na huduma mpya zilizopo sokoni.
Msanii maarufu anayetesa na wimbo wake wa ‘segere’ Siza Mazongela
akikonga nyoyo za mashabiki wake katika tamasha la Uhondo wa Zantel
lililofanyika katika viwanja vya Temeke Mwisho, Dar es Salaam
ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu yamkononi ya Zantel kuwa
karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma mpya zilizopo
sokoni.

No comments: