Mchungaji King James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) kutoka Maeneo ya Kahororo Kyamaizi Bukoba, King James ambaye pia ni mmoja wa wadau mmoja wa wadau wa maendeleo Manispaa ya Bukoba Leo jumatano septemba 14, 2016 jioni amewatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Wananchi. Ni baada ya maafa kutokea katika janga la tetemeko la ardhi, lililotokea jummosi iliyopita mkoani hapa Kagera, ambapo imeripotiwa idadi ya vifo kuongezeka na kufikia watu 17, huku wengine 253 wakijeruhiwa na kusababisha simanzi na masikitiko kwa familia nyingi. Katika tukio hilo, pia nyumba 840 za makazi zimeanguka, nyumba 1,264 zimepata nyufa kubwa na majengo 44 ya taasisi mbalimbali zikiwemo shule kuanguka.
King James ametembele sehemu tofauti tofauti kama Kata ya Hamugembe, Kashai, Rwamishenye na kutoa Misaada ya dharura kama Mahema, mchele, Sukari na Pesa taslimu na kuwaombea pia. Mchungaji James pia kesho ataendelea kutoa Misaada kwa Wahanga wa Tetemeko la Ardhi la nguvu ya 5.7 katika vipimo vya Richter lilitokea eneo la Bukoba, kaskazini magharibi mwa Tanzania ambalo limeathiri sehemu kubwa ya Wanakagera kuanzia kwenye Makazi yao na wengine kukosa makazi na mpaka sasa kulala nje kutokana na nyumba zao kubomolewa.
Takribani shilingi bilioni 1.4 zimepatikana mpaka sasa katika harambee iliyoongozwa na serikali ili kusaidia athari za tetemeko la ardhi hapa mkoani Kagera. 
Hamugembe Omukishenye ni sehemu kubwa iliyoathiriwa na tetemeko la Ardhi na Nyumba Nyingi kuanguka na nyingi kubomoka huku ikiwa imepoteza zaidi ya Wakazi 6.
Furaha kwa Mama Saada mama Mlezi wa Watoto Yatima baada ya kutembelewa na kupokea Misaada, Na hapa akiwashukuru wageni hao waliompatia msaada huo wa Dharura katika kipindi hiki kigumu kinachowalaza nje baada ya Nyumba yao kuangushwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea Jumamosi septemba 10, 2016.
No comments:
Post a Comment