Wednesday, September 7, 2016

SIMU TV: habari kutoka televisheni

SIMU.TV: Mahakama nchini imesema ipo tayari kupokea majaji wapya ili kupunguza mrundikano wa kesi na ucheleweshwaji wa hukumu. https://youtu.be/-f6bLbSGQKw

SIMU.TV: Upotevu wa mapato na mwingiliano wa raia wa Kenya na Tanzania katika mpaka wa kijiji cha Njoroi wilayani Loliondo umesababishwa na kukosekana kwa kituo cha pamoja cha forodha.
Makamu wa rais Bi Samia Suluhu Hassan amesema serikali itatuma kikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na uvuvi haramu katika bahari. https://youtu.be/5Wra8ZSVcF0

SIMU.TV: Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam inakabiliwa na ukosefu wa chumba cha upasuaji na ukosefu wa vifaa tiba vya upasuaji. https://youtu.be/8QB9M7TGtLk

SIMU.TV: Wizara ya maliasili na utalii yawataka wananchi wanaofanya shughuli mbalimbali katika maeneo ya hifadhi kinyume na utaratibu kuondoka mara moja.https://youtu.be/4EVP05Ox7E8

SIMU.TV: Wanafunzi wa darasa la saba katika shule za msingi nchini leo wameanza mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ambao utafanyika kwa siku mbili.https://youtu.be/FiixBvyBhh0

SIMU.TV: Wananchi wilayani Hanang wameaswa kuchangamkia fursa ya kuwepo kwa soko la mazao la kimataifa ili kuweza kujikwamua kiuchumi. https://youtu.be/P77CDFd8Xb0

SIMU.TV: Vijana wajasiriamali wanaofanya biashara ya bodaboda wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani ili kulinda afya za wateja wao. https://youtu.be/p58V_cS7jCU

SIMU.TV: Jumuiya ya wafanyabiashara wa halmashauri ya Rungwe wameiomba serikali kutoa bei elekezi ya ulipaji wa kodi ili kuwawezesha kulipa kodi kwa wakati.https://youtu.be/4_DjzMdz5rc

SIMU.TV: Simba imeibuka mbabe mbele ya timu ya Ruvu Shooting baada ya kuichapa mabao mawili kwa moja na kuiwezesha simba kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi. https://youtu.be/K1cOgTbU5ZY

SIMU.TV: Wadau wa soka wilayani Maswa waiomba serikali kutatua changamoto ya viwanja vya michezo katika wilaya hiyo. https://youtu.be/DzsxUtYxb1s

SIMU.TV: Uwiano usioridhisha wa kijinsia katika uongozi wa sekta ya michezo nchini umetajwa kuwa changamoto inayokabili maendeleo ya michezo kwa wanawake.https://youtu.be/_6uuGgPJO24

SIMU.TV: Mshambuliaji wa Manchester United Marcos Rashford ameifungia timu ya vijana ya Uingereza mabao matatu kwenye mchezo wa kufuzu mataifa bingwa ya Ulaya.https://youtu.be/ZxCap-Ju7v4

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa, ametembelea makazi na ofisi yake binafsi zinazojengwa mkoani Dodoma na kutoa utaratibu utakaotumika kuhamishia serikali mkoani humo; https://youtu.be/g0qt8_tz6n8

SIMU.TV: Tanzania imekataa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara ule unaozihusisha nchi za Afrika mashariki pamoja na Umoja wa ulaya yaani EPA;https://youtu.be/a52ujJtipXU

SIMU.TV: Wakati mitihani ya kumaliza kwa elimu ya msingi ya darasa la saba ikiendelea, haya hapa maoni ya baadhi ya wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali nchini;https://youtu.be/EuA3Wvqcj54

SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu. amesema serikali itatuma kikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na uvuvi haramu huko mkoani Mtwara;https://youtu.be/z1ppWFPKGMs

SIMU.TV: Watumishi 34 wa mahakama nchini, wamefukuzwa kazi baada ya tume ya maadili ya mahakama kujiridhisha kuwa walikiuka maadili ya kazi;https://youtu.be/fIq43MyCvHA

SIMU.TV: Baadhi ya wabunge katika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, limeshauri muswada wa upatikanaji wa habari uweke wazi aina gani za habari zinapaswa kutumwa; https://youtu.be/u_fLrKXSAaw

SIMU.TV: Wazee katika kambi ya kulelea wagonjwa ukoma wilayani Manyoni, wanaishi katika mazingira magumu kutokana na kukosa huduma muhimu za chakula na dawa;https://youtu.be/2vFqWcPjjgE

SIMU.TV: Benki kuu ya Tanzania imefanikiwa tuzo 2 kutoka kwa jumuiya ya kimataifa inayojihusisha na utoaji huduma za kifedha; https://youtu.be/o35_Wjk9KM0

SIMU.TV: Wafanyabiashara nchini wametakiwa kurasimisha biashara zao ili ziweze kutambulika na kuchangia ukuaji wa uchumi wan chi yetu; https://youtu.be/6Kz37AllMtA

SIMU.TV: Kampuni ya mafuta ya Total imezindua kilainishi cha vyombo vya moto yaani magari na pikipiki ili kuweza kuwezesha kufanyakazi kwa wamiliki wa vyombo hivyo kwa uhakika; https://youtu.be/enNbPgCcvuw

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Mlelo Rachel Kasanda, amewaomba wamiliki wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom kuwasaidia pesa watu masikini wilayani humo;https://youtu.be/k459gQHAuGs

SIMU.TV: Timu ya soka ya Simba, imendelea kulifukuzia taji la ligi kuu msimu huu baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Ruvu shooting mabao 2-1  katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es salaam; https://youtu.be/_ZwD3GraxME

SIMU.TV: Timu ya mpira wa miguu ya Bunge, inatarajia kushuka dimbani na viongozi wa dini mwishoni mwa wiki hii mkoani Dodoma; https://youtu.be/R5R1YDiotbw

SIMU.TV: Michuano ya kuwania kufuzu kombe la dunia hapo 2018 nchini Russia iliyopigwa hapo jana, huu hapa mchanganyiko wa matokeo kwa mechi zilizopigwa hapo jana;https://youtu.be/EuA3Wvqcj54

SIMU.TV: Kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake Sebastian Nkoma, amesema wachezaji wake wanaendelea na mazoezi huku wakiwa na hali nzuri kabisa;https://youtu.be/g_Vkcd-NLN4


No comments: