Eleuteri
Mangi na Batrice Lyimo-Dodoma
Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa wa
mwaka 2016 ili ufuate hatua ya kusainiwa na Rais akiwa sehemu ya Bunge ili
uweze kuwa sheria kamili itkayotumika Tanzania Bara.
Hatua hiyo imefikiwa
baada ya kamati ya Bunge zima kumaliza kazi yake saa 2:15 usiku ya kupitia
kifungu kwa kifungu na kukubali pamoja na marekebisho yake.
Awali kwa upande wa
Serikali wakijibu hoja za Wabunge kuhusu Muswada huo walisema utasaidia kupanua
wigo wa upatikanaji wa taarifa, utasaidia kukuza tasnia ya habari, utakidhi
hitaji la Kikatiba la watu kupata taarifa.
Upande wa Serikali
uliwakilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerge Masaju, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu (Watu Wenye
Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi
Kupitishwa kwa
Muswada huo ni kutekeleza matakwa ya kifungu cha Sheria cha 18 cha Katiba ya
nchi ambacho kinatoa haki ya mtu kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio
mbalimbali ya nchi na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha ya shughuli za
maisha ya wananchi na masuala ya kijamii.
Aidha, Muswada huo
utasaidia upatikanaji wa taarifa ambazo ni nyenzo muhimu na chachu ya maendeleo
ya taifa.
Muswada uliopitishwa leo
na Bunge mjini Dodoma umejadiliwa kwa muda wa siku mbili ambapo jumla ya
Wabunge 44 wamechangia hoja wakati wa mjadala, Wabunge 39 wametoa michango yao
kwa njia ya kuongea wakati wa Bunge na Wabunge watano wamechangia hoja zao kwa
maandishi.
No comments:
Post a Comment