Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili
katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo
akitokea Unguja kwa ziara kikazi kisiwani humo akiwa na ujumbe
aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwemma Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na MkeweMama Mwanamwema Shein wakisalimiana na
Viongozi mbali mbali wakati walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba
leo kwa ziara maalum kisiwani humo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa
KMKM Pemba wakati alipofika katika kituo kikuu cha karafuu cha ZSTC Wete Pemba
kuangalia karafuu zilizokamatwa katika Bandari ya Tondooni Mkumbuu Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba,alipofanya
ziara maalum leo,(wa pili kulia) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Bi.Amina
Salum Ali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa
Mdhamini wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Nd,Abdalla Ali Ussi (kushoto)
alipotembelea kituo kikuu cha karafuu cha ZSTC Wete Pemba kuangalia karafuu
zilizokamatwa katika Bandari ya Tondooni
Mkumbuu Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba leo alipofanya ziara maalum
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa
Biashara,Viwanda na Masoko Bi.Amina Salum Ali (katikati) wakati alipotembelea
kituo kikuu cha karafuu cha ZSTC Wete Pemba baada ya kuangalia karafuu
zilizokamatwa katika Bandari ya Tondooni
Mkumbuu Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba,akiwa katika ziara ya kikazi
kisiwani humo,(kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko
Nd,Bakari Haji Bakari
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa
Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma (wa pili kushoto) wakati
alipotembelea Uwanja wa Mpira wa Gombani kuangalia matengenezo makubwa yaliyomalizika
kwa utiaji wa (Tatan) ambapo sasa Uwanja huo utaweza kutumika kwa shuhuli mbali
mbali za michezo ikiwemo Riadha,(kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu),
Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment