Saturday, September 10, 2016

Bonanza la uzinduzi wa Michezo ya 34 ya SHIMIWI Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam


 Mgeni rasmi Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean  Ndumbaro (watatu kushoto) akimkabidhi kombe mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Wizara hiyo kushika nafasi ya pili wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru. Waliosimama kushoto na kulia ni baadhi ya viongozi wa Wizara na Taasisi za Umma


Mgeni rasmi Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurence Ndumbaro (watatu kulia) akimkabidhi kombe mwakilishi kutoka ofisi ya Jiji la Dar es Salaam kwa Jiji kushika nafasi ya kwanza wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru. Waliosimama kushoto na kulia ni baadhi ya viongozi wa Wizara na Taasisi za Umma 
 Viongozi kutoka Wizara na Taasisi za Umma katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati mwenye suruali ya kijani) wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru.
 Watumishi kutoka ofisi ya Jiji la Dar es Salaam wakishangilia ushindi wa kwanza huku wakionyesha zawadi ya kikombe cha ushindi wakati wa Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru

Madaktari wa wanamichezo wakitoa huduma ya kwanza kwa utumishi wa umma aliyeumia wakati akishiriki Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya 34 ya Shimiwi leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru
Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, leo wameshiriki katika Bonanza Maalumu la Michezo ya SHIMIWI kwa watumishi wa Umma, ambalo limefanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Katika Bonanza la leo Mgeni rasmi alikuwa ni Katibu mkuu Utumishi, akimwakilisha Katibu mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambao wameshiriki Bonanza la Michezo ya SHIMIWI liliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, wakiwa wamepozi katika Picha ya pamoja. 
Waliosimama Kutoka Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Dkt Kusiluka, Mkurugenzi wa ICT Eliasi Nyabusani pamoja na Msajili wa Hati Subira Sinda wakibadilishana Mawazo leo wakati wa Bonanza la Michezo la SHIMIWI kwa watumishi wa Umma  lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa ICT Eliasi Nyabusani ( katikati ) na Mwenyekiti wa Michezo wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndugu Swagile Msananga wakiwa Sambamba na Katibu ndugu Mwikari Mshana wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kwenye Uwanja wa Uhuru.

No comments: