Thursday, September 1, 2016

MAANDALIZI YA ENEO LA RUJEWA MBARALI LITAKAPOPATWA JUA

 Mafundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakirekebisha   kifaa kwenye nguzo watakapoweka mitambo ya kurusha matukio moja kwa moja duniani kutoka eneo la Rujewa, wilayani Mbarali, Mbeyai patakapokuwa na tukio la Kupatwa kwa Jua leo. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA:KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Wilaya hiyo, John Kalla akichora vibao kuanisha maeneo
 Baadhi ya watoto waliokutwa eneo hilo wakiwa na furaha tukio hilo kufanyika wilayani humo.
 Mkazi wa Rujewa mwenye jamii ya kimasai, Joshua Ole Kaulule, alijibu kuwa  anachojua ni kwamba leo, jua na mwezi vitagongana na kusababisha giza zaidi ya hapo haelewi.
 Maeneo yakifyekwa eneo hilo ikiwa ni sehemu ya maandalizi
 Jamaa akiandaa vibanda vya biashara
 Pepsi nao hawakuwa nyuma kuweka kibanda chao
 Mwandishi wetu alipata wasaa wa kuzungumza na Pasvolo Mwinuka Mwalimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Idara ya Sayansi,  ambaye alieleza kitaalamu juu ya kupatwa kwa jua.

Mwandishi wetu alipata wasaa wa kuzungumza na Pasvolo Mwinuka Mwalimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Idara ya Sayansi,  ambaye alieleza kitaalamu juu ya kupatwa kwa jua.

Alisema kuwa tukio hilo hutokea dunia, mwezi na jua vinapokuwa kwenye mstari mmojo na mwezi kuwa kati hivyo kuziba mwanga jua kuifikia dunia.

Alitaja aina tofauti za kupatwa kwa jua kuwa ni. Mosi; Kuziba kabisa mwanga wa jua kunaitwa kupatwa kwa jua kikamilifu (Total Solar Eclipse).

Pili;Kiasi kidogo cha mwanga wa jua kuifikia dunia (Partial Solar Eclipse) na miale ya jua itakuwa imezibwa kwa kiasi kikubwa kwa asilimia 97, kitendo ambacho hutengeneza muonekano wa mfano wa pete na tukio hili ndiyo litakalotokea leo Rujewa. Kupatwa kwa jua kutaanza saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Alisema kitendo hicho duniani kitatokea hapa nchini eneo la Relini Rujewa, mkoani Mbeya na kutaja  maeneo mengine patapoonesha kwa kiasi tukio hilo ni wilayani Wanging'ombe, Njombe, Karibu na Ziwa Tanganyika pamoja na baadhi ya Nchi ya DRC Congo.


 Kampuni ya Simu wakiendelea na kazi


 Choo cha muda kikijengwa

 Mariam alipelekwa eneo hilo na wenzake lakini bila kujua kitakachojiri
 Lakini Mwananfunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Ibala, Adamu Chengula alikiri somo hilo kufundishwa, hivyo kujibu kiufasaha kwamba kupatwa kwa jua ale inapotokea  Dunia, Mwezi na Jua kuwa kwenye mstari mmoja na mwezi ukiwa katikati huzuia miale ya jua na kusababisha giza katika uso wa dunia.

 mfanyabiashara wa mchele, Heri Kiluswa, alisema kuwa yeye alikuwa anapita barabarani alishawishiwa kwenda pale baada ya kuona watu wengi wamekusanyika, lakini haelewi ni kitu gani kitanyika na alipouliza aliambiwa kuwa kuna tukio la kupatwa na jua, ila bado haelewi ni jambo gani.
 Naye Halima Abbas (35) ambaye ana elimu ya sekondari kidato cha nne, alisema kuwa anasikia tu kwamba kuna kupatwa kwa jua lakini hajui ni kitu gani. Pia alisema hakumbuki kama somo hilo alilisoma akiwa shuleni.

 Mwanafunzi wa Darasa la saba katika Shule ya Msingi Ihanga, Goodluck Mwanpasha (13), alisema kuwa hajui lolote na hata shule hajawahi fundishwa na baada ya kuona watoto wenzie wanamcheka alitimua mbio na kutokomea.

 Baadhi ya wananchi wkiwa eneo ambalo Jua litapatwa na mwezi
 Vibanda vya biashara vikijengwa eneo hilo
 Biashara ya vinywaji ikiendelea katika eneo hilo
Jumanne Mavunde (45), aliyekutwa akiwa amejiinamia kwenye baiskeli yake, alisema kuwa hata yeye hajui kitakachotukia ila alisikia alipofika pale kuwa eti jua litapatwa na kwamba walioandaa ndiyo wanaojua.

No comments: