Wednesday, August 31, 2016

MWENYEKITI WA BODI YA UTALII (TTB) AWAAGA WATALII NA WAANDISHI WA HABARI WANAOKWENDA RUJEWA KUSHUHUDIA KUPATWA KWA JUA

1
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akiagana na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena Kiongozi wa Msafara wa Watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaotoka Dar es salaam kwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua ambapo wageni mbalimbali pamoja na wanahabari kutoka vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa wako mkoani humo kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo nadra kutokea duniani.
2
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi wakiagana na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena pamoja na Antonio Nugas Mtembezi kutoka Clouds Media Viongozi wa Msafara wa Watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaokwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
3
Baadhi ya wapiga picha wa vyombo vya habari hapa nchini wakiendelea na kazi yao wakati msafara huo ukiondoka jijini Dar es salaam.
4
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi. Devotha Mdachi wakielekea kwenye gari kwa ajili ya kuwaaga baadhi ya watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaokwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua wakitokea jijini Dar es salaam..
6

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari na kuwapa maneno kadhaa wakati akiwaaga baadhi ya watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaokwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua wakitokea jijini Dar es salaam
7 8
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari, kulia ni Bi. Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB na kutoka kushoto ni Mtangazaji wa Clouds Baby Kabaya na Mkurugenzi wa Masoko TTB Bw. Philip Chitaunga,
10
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akiasalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Utalii TTB.
12
Kulia ni Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena na kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TTB Bw. Geofrey Tengeneza na Mkurugenzi wa Masoko TTB Bw. Philip Chitaunga.

1 comment:

Steve Lazaro said...

Nimependa utalii wa ndani na hasa baada ya TTB kutumia usafiri wa Rungwe Express ili kuitangaza Rungwe kama kivutio cha watalii kwa kuwa na Milima mirefu, Mito na chemichemi za ajabu nk mkoani mbeya