Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu kwa wanamichezo ambao ni walimu wanaowakilisha nchi za kusini mwa Afrika wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kushoto ni Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.
Kikosi cha Brass Bendi ya Polisi Nchini wakiongoza maandamano ya wanamichezo ambao ni walimu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kuingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo Jijini Dar es Salaam.
Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Zambia wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo JijiniDar es Salaam.
Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Afrika ya Kusini wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.
Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Tanzania wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika
(SATO) leo Jijini Dar es Salaam.Picha
Na: Lorietha
Laurence WHUSM.
Lorietha
Laurence - WHUSM
Michezo
ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kuimarisha ushirikiano na mahusiano baina ya nchi na nchi.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye wakati wa ufunguzi wa michezo ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za
Kusini mwa Afrika (SATO) ambayo imeanza rasmi leo Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Nnauye amesema kuwa ni fahari kubwa kwa serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa
mashindano hayo kwa kuwa inatoa fursa kwa wageni na wenyeji kujumuika kwa
pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kimichezo.
“Kuunganisha
nchi na nchi si kazi rahisi lakini kupitia michezo imekuwa ni jambo rahisi kwa
kuwa inawafanya kuwa na umoja uliothabiti na hivyo kuimarisha mahusiano baina ya
nchi husika” alisema Mhe. Nnauye
Aidha
Mhe. Nnauye aliwataka washiriki wasiishie kwenye michezo tu bali pia watumie fursa ya kuwepo nchini kwa kutembelea vivutio
mbalimbali vilivyopo katika Jijini la Dar es Salaam ikiwemo Makumbusho ya Taifa
pamoja na Bagamoyo ambako kuna historia kubwa ya nchi.
Naye
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba ameeleza kuwa mashindano
hayo ni muhimu kwa walimu kwa kuwa yanawasiadia kuimarisha afya pamoja na kushirikiana
katika kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.
“kupitia
michezo hii tunaimarisha afya pamoja na kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo walimu ikiwemo
ukosefu wa walimu wa masomo ya hesabu na sayansi na namna ya kutatua tatizo
hilo “ alisema Bw. Mukoba.
Kwa
upande wake Rais wa Vyama vya Walimu wa
Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda amesema kuwa kupitia michezo
hiyo walimu hujifunza tamaduni mbalimbali baina yao ukizingatia elimu ndio msingi
wa maendeleo.
Mashindano
haya ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO)
yanafanyika kwa mara ya sita huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo
kwa mara ya kwanza ikihusisha nchi za Namibia, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Zambia,
Malawi, Afrika ya Kusini, Swizland na Tanzania.
No comments:
Post a Comment