Tuesday, August 30, 2016

Kampuni ya TTCL yajitosa Miss Higher Learning Institutions 2016.

 Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga akizungumza na washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 pamoja na wageni wengine walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo. Nyuma yake ni washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016. Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga akizungumza na washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 pamoja na wageni wengine walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo. TTCL ndiye mdhamini mkuu wa shindano la Miss Higher Learning Institutions kwa mwaka 2016. Mkuu wa Hitifaki Kamati ya Miss Tanzania 2016, Albert George Makoye (wa kwanza kushoto) akizungumza kutoa shukrani kwa kampuni ya TTCL kwa kukubali kuwa mdhamini mkuu wa Miss Higher Learning Institutions 2016. Wengine ni viongozi na washiriki wa TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016. TTCL ndiye mdhamini mkuu wa shindano la Miss Higher Learning Institutions kwa mwaka 2016. Mratibu wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Bi. Maya Nkiru (kushoto) akizungumza kuishukulu kampuni ya TTCL kwa kukubali kuwa mdhamini mkuu wa shindano hilo. Kulia ni Meneja Masoko wa TTCL, Beda Kinunda akiwa katika hafla hiyo. Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga (kulia) akiwagawia line za TTCL zenye huduma za 4G LTE kwa baadhi ya washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo. TTCL ndiye mdhamini mkuu wa shindano la Miss Higher Learning Institutions kwa mwaka 2016. Washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakiwa katika pozi walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo. Mkuu wa duka la huduma za TTCL Makao Makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam, Diana Obed (kulia) akitoa maelekezo kwa washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 juu ya bidhaa na huduma mbalimbali za TTCL zinazopatikana katika duka hilo. Meneja wa Biashara wa TTCL Mkoa wa Dar es Salaam, Augustino Mwakyembe (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 walipotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja cha TTCL Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo.


 Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) wameingia kama mdhamini mkuu wa mashindano ya urembo kutafuta mrembo toka vyuo vikuu nchini 'TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016' atakaye shiriki katika fainali za urembo kumpata mlibwende wa Tanzania 2016.

 TTCL wametangaza kuingia katika udhamini huo leo jijini Dar es Salaam ambapo warembo wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 walipotembelea Makao Makuu ya TTCL kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na shirika hilo la umma nchini Tanzania.

 Akizungumza katika tukio hilo Meneja Huduma kwa Wateja wa TTCL, Aron Msonga amesema shirika hilo limevutwa kusaidia mashindano hayo ili kuweza kuwapata warembo wenye sifa stahiki watakao shinda katika kinyang'anyiro cha 'TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016' na baadaye kushiriki shindano la Miss Tanzania 2016. 

Amesema TTCL kwa sasa inafanya mageuzi makubwa ya kibiashara na uendeshaji ambayo yameboresha huduma za shirika hilo na bidhaa zake kwa ujumla yanayoinufaisha jamii, hivyo haiwezi kujitenga na shughuli za kijamii ikiwemo mashindano ya urembo. 

Aidha amewashauri waandaaji wa TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 kufuata taratibu zote bila upendeleo ili kuweza kuwapata wawakilishi wasomi na wenye sifa za ulimbwende ambao watashiriki vema katika kumpata Miss Tanzania 2016. 

Kwa upande wake Mratibu wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Bi. Maya Nkiru ameishukuru kampuni ya TTCL kwa kuunga mkono mashindano hayo na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha yanafanyika kwa mafanikio makubwa na hatimaye kupatikana warembo wenye vigezo na sifa kuwakilisha tawi hilo kwa ufasaha. Mratibu huyo alisema shindano la kumpata mrembo atakayewakilisha 'TTCL Miss High Learning 2016' kwa mwaka huu limeboreshwa na litakuwa na burudani za kutosha na utofauti mkubwa hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuweza kushuhudia shindano hilo. Aidha alitaja baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika shindano hilo kuwa ni pamoja na msanii Ney wa Mitego, MB Dog, Msaga Sumu na kundi la QS. TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 itafanyika Septemba 17, 2016 katika Ukumbi wa TTC Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

No comments: