Tuesday, August 2, 2016

TRENI YA PILI YA JIJINI DAR KUANZIA STEHENI HADI PUGU YAANZA SAFARI ZAKE

 Treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ikiwa tayari kwa kuanza safari yake ya Jiji kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam kwenda Pugu huduma ambayo imeanza kutolewa rasmi jana.
TRENI ya pili ya Jiji la Dar es salaam imeanza kutoa huduma zake kwa safari  za jiji za kuanzia Stesheni hadi pugu, ambayo itakuwa ikitoa huduma mara 3 kwa asubuhi na mida ya jioni mara 3 ambayo itasaidia sana kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo huku ikiongeza kasi ya uchumi kwa wakazi wa maeneo ya pugu hasa wakiwemo wachuuzi.

Baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo wanaotokea maeneo ya kuanzia kipawa mpaka Pugu, wamepngeza kuanzishwa kwa safari hiyo, kwani itawapunguzia adha ya safari ya muda mrefu njiani na sasa watakuwa wakiwahi katika maeneo yao ya biashara hasa wale wanaofika Soko la Kimataifa la Samaki Ferry kuchukua Samaki, ambapo sasa watachukua usafiri wa Bajaji na kuwahi usafiri wa treni kwa muda uliopangwa.
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakigombania kuingia katika mabehewa baada ya kuanzishwa usafiri huo.


Wanafunzi wa Shule Mbalimbali wakiwa ndani ya mabehewa ya Treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) katika Stesheni ya Dar es Salaam kwenda Pugu huduma ambayo imeanza kutolewa. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)




Askari wa kike ambae jina lake halikuweza kupatikana maramoja, akidandia behewa huku Treni ikiwa imeanza mwendo katika kituo ya Buguruni.

No comments: