Tuesday, August 16, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kama machinga wameanza tena kurejea katika eneo la Msimbazi Kariakoo ambapo waliondolewa miezi michache iliopita.https://youtu.be/Rme6y6X6H1Y

Mamlaka ya mapato TRA imewataka wafanyabiashara wote waliojisajili katika mamlaka hiyo kama walipa kodi kufika katika mamlaka hiyo kuhakiki kumbukumbu zao.https://youtu.be/rQbZEVeN4k8

Baadhi ya wafugaji katika wilaya za mkoa wa Morogoro wameendelea kuhoji nia ya serikali kufanya sensa ya mifugo na kusema watengewe kwanza maeneo ya malisho.https://youtu.be/YjhYdDfSwhk

Wadau wa elimu leo wamekabidhi hundi kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ikiwa ni juhudi za kuunga mkono zoezi la uchangiaji wa madawati.https://youtu.be/5z0hYuA70s8

Kamati ya maridhiano Tanzania inayoundwa na viongozi wa dini mbalimbali nchini imetoa wito kwa serikali na vyama vya upinzani kukaa pamoja na kutafuta suluhu badala ya kuruhusu maandamano. https://youtu.be/jUWwrnx7jHY

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amempa siku saba mkandarasi anaetengeneza barabara za mitaa kutoa matofali yaliyojengwa chini ya kiwango.https://youtu.be/6471SxjoLig

Vero Doto mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Muhimbili two anaomba msaada kwa wasamaria wema kumsaidia kupata vifaa vitakavyomwezesha kusoma kutokana na matatizo yanayomkabili. https://youtu.be/wQzZOWPxAMY

Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania TPA imesema itachukua hatua za kuhakikisha kuwa tatizo la kushuka kwa shehena ya mizigo katika bandari ya Dar es Salaam linakwisha.https://youtu.be/qeGpqi42ZAo

Wajasiriamali mali wadogo wanaopata mikopo kutoka benki ya biashara ya Mkombozi wameanza kunufaika na huduma za bima ya afya. https://youtu.be/pG4GUZZFx2I

Azam Fc na Yanga kesho zinatarajia kufungua pazia la ligi kuu ya soka nchini kwenye mchezo wao wa ngao ya jamii ambapo kampuni ya TING imepata haki ya kuonesha mchezo huo. https://youtu.be/n9tQTPgqMUk

Baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga wameandamana hadi makao makuu ya klabu hiyo wakipingana na kauli za wanachama wanaodaiwa kumkashifu mwenyekiti wa klabu hiyo. https://youtu.be/zDIWI8mWEo8

Timu ya Ndanda fc imemchukua mkurugenzi wa benchi la ufundi la timu hiyo kukaimu nafasi ya kocha baada ya kukimbiwa na kocha wake. https://youtu.be/BgDTEBIP4eM

Mwanariadha wa Kenya David Rudisha ameonesha uzoefu wa hali ya juu baada ya kushinda mbio za mita mia moja kwenye mashindano ya Olympic huko nchini Brazil.https://youtu.be/N6md4VOYVrs

No comments: