Na John Stephen
Dar es Salaam, Tanzania.
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan LEO ameitembela Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete na kuahidi kutoa mafunzo kwa wataalamu wa taasisi hiyo.
Balozi huyo ametembelea
chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na vyumba vya upasuaji pamoja
na kuwaona wagonjwa wodini.
“Nimefurahishwa kusikia
kuna madaktari ambao wamesoma Israel na ninapenda kuwaahidi kuwa Serikali yangu
itaendelea kuisaidia tasisi hii, lakini sitatoa hela,” amesema LEO.
Pia amesema kuwa
anafarijika kuona shughuli za kitabibu zinazofanywa na taasisi hiyo kwa kuwa
amekuwa akitaka kwenda kuitembelea lakini hakuwahi kupata nafasi hivyo
amefurahi kupata fursa hiyo.
Wakati huo huo huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema
wanakabiliwa na upungufu wa wataalamu sawa na asilimia 50.
“Tunahitaji wataalamu 278,
sasa tuna wataalamu 147 kwa mfano tuna wauguzi 96, mahitaji halisi ni wauguzi
150,” amesema Profesa Janabi.
Katika hatua nyingine,
Profesa Janabi amesema hospitali hiyo tayari imewafanyia upasuaji zaidi ya
watoto 600 kuanzia mwaka jana hadi sasa.
Profesa Janabi amesema
taasisi hiyo imewekeza zaidi katika kununua vifaa tiba vya kisasa na
kuwawezesha madaktari na wauguzi kupata mafunzo kutoka nje ya nchi ikiwamo
Israel.
Amesema kuwa mpango
huo umesaidia wagonjwa wengi kufanyiwa upasuaji ambao umekuwa
ukifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.
Baadhi ya wageni waliowahi
kutembelea taasisi hiyo ni mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini
Tanzania, mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria na mchezaji wa
kimataifa, Nwankwo Kanu na madaktari kutoka nchi mbalimbali
ambao wamekuwa wakishiriki katika upasuaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kulia) akimkaribisha Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan wakati alipotembelea taasisi hiyo LEO.
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akisikiliza ripoti ya shughuli za kitibabu zinazotolewa na taasisi hiyo kutoka kwa Profesa Mohamed Janabi.
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kulia) wakiingia katika chumba cha upasuaji LEO katika taasisi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji JKCI, Dk Bashir Nyangasa akifafanua jambo kwa balozi huyo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akizungumza na madatari, wauguzi na wataalamu wengine wa taasisi hiyo
Madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wakimsikiliza Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan kwenye taasisi hiyo.
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan (kulia) akisaini kitabu cha wageni kabla ya kupata taarifa fupi ya taasisi hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi.
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akizungumza na madatari, wauguzi na wataalamu wengine wa taasisi hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza kwenye mkutano huo
Dk Peter Kisenge akimkabidhi zawadi balozi huyo
Wafanyakazi wa taasisi hiyo wakiwa katika picha pamoja na mgeni huyo. Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
No comments:
Post a Comment