Tuesday, August 2, 2016

NAIBU WAZIRI SULEIMANI JAFFO AHIMIZA USAFI KWENYE MAJIJI,AKAGUA MAGARI MAALUMU JIJINI ARUSHA LEO.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kusimamia na kutumia mitambo na magari ya kisasa ya kukusanya Taka ngumu kwenye majiji na halmashauri zilizopo kwenye mpango wa kuendeleza miji kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya Rais kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia,kushoto ni Mratibu wa Mradi huo,Mhandisi Davis Shemangale na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya usimamizi miundombinu ya ukusanyaji Taka ngumu wakimsikiliza Naibu Waziri,Suleimani Jaffo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo(aliyevaa tai nyekundu) akiwa ujumbe ofisi yake na watumishi wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakati akikagua eneo lililotengwa kwaajili ya kuchomea taka ngumu lilipo Dampo Kuu jijini humo katika mpango wa kuendeleza miji kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya Rais.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akikagua Dampo la Jiji la Arusha liliboreshwa miundombinu yake kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Sehemu ya magari maalumu yatakayohusika kukusanya Taka ngumu kutoka mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha.

Naibu Waziri Jaffo alitaka mitambo hiyo itumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kufanyiwa matengenezo kila mara ili iwe endelevu na kuongeza kuwa serikali imeshaweka mikakati ya miji yote kuwa misafi.

No comments: