Imeelezwa kuwa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma utakamilika
mwishoni mwa mwezi Agosti ili kuruhusu ndege za abiria sabini mpaka tisini kuweza
kutua na kuruka na hivyo kurahisisha usafiri wa anga kwa ukanda wa kati.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa baada ya kutembelea kiwanjani hapo kukagua hatua ya mwisho ya ujenzi
iliyofikiwa ambapo amesema kasi ya Mkandarasi Chicco anayetekeleza kazi hiyo
inaridhisha katika kuhakikisha kiwanja hicho kinakamilika kwa muda na kwa viwango
vilivyokubalika.
Amesema mpaka sasa ni asilimia themanini ya kazi iliyotekelezwa kwa siku arobaini na
tano tangia kuanza ukarabati hivyo kasi iliyotumika kwenye kiwanja hiki itatumika
kwenye ujenzi wa viwanja vingine nchini.
"Tunaamini kabisa kwa kasi ya mkandarasi na msimamizi mtakamilisha ujenzi huu
haraka na viwango tulivyokubaliana katika mkataba ili ndege kubwa zianze kutua na
kuruka" amesema Prof. Mbarawa.
Naye Msimamizi wa ujenzi wa kiwanja hicho kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) Eng. Mhandisi Mbila Mdemu amesema kazi ya ukarabati na upanuzi
inaendelea kufanywa usiku na mchana kwa kuzingatia ubora na viwango na kukamilika
kwa wakati
"Tulipewa kazi hii na tunaahidi kuwa itakamilika kama tulivyoelekezwa ili kuwapa
wananchi wanaozunguka mikoa ya Dodoma na jirani fursa ya kutumia usafiri wa Anga",
amesema Eng. Mdemu.
Ameongeza kuwa kazi zinazokamilishwa sasa ni kumalizia sehemu ya maegesho ya
ndege na tabaka la mwisho kwenye barabara ya kuruka na kutua ndege.
Mradi wa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umegharamiwa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zaidi ya shilingi bilioni 11.8 na
kukamilika kwake kutaongeza idadi ya safari za ndege zitakazosafirisha abiria wa mikoa
ya kanda ya kati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa
ya maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma kutoka kwa
Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho, Mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa kutoka Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja
hicho Mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa vitendo wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa
kiwanja cha ndege cha Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuka kutoka
kwenye katapila mara baada ya kukagua vifaa vya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha
ndege cha Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa mmoja wa mafundi wanaokarabati na kupanua kiwanja cha ndege cha
Dodoma wakati alipokagua kiwanja hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa mmoja wa mafundi wanaokarabati na kufanya upanuzi katika kiwanja
cha ndege cha Dodoma wakati alipokagua kiwanja hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa katika
picha ya pamoja na mafundi wanaokarabati na kufanya upanuzi wa kiwanja cha ndege
cha Dodoma wakati alipokagua kiwanja hicho.
No comments:
Post a Comment