Friday, August 19, 2016

HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi, amefuta hati ya umiliki wa ardhi kwa kampuni ya Rockshield Quality iliyopo wilayani Misenyi mkoani Kagera; https://youtu.be/__lUEQu0X8Q

SIMU.TV: Baadhi ya viongozi wa dini akiwemo mwenyekiti wa kamati ya amani mkoani wa Dar Es salaam sheikh Mussa Salum wameitaka jamii kuachana na matendo yatakayopelekea kuhatarisha amani ya nchi; https://youtu.be/7R3Jd7M_Om4

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli ambae pia ni mwenyekiti wa jumuiya ya afrika mashariki, amekutana na katibu mkuu wa jumuiya jijini Dar Es salaam na kumuhasa anahakikisha jumuiya hiyo inabana matumizi; https://youtu.be/I9X4lHOTsBM

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli amemkabidhi pikipiki yenye matairi matatu  maarufu kama Bajaj mlemavu wa miguu anayetumia baiskeli aliyemuahidi baada ya kumuona katika taarifa ya habari; https://youtu.be/i1GQe8DO-8A

SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu, ametoa wito kwa wakadiriaji wa majengo kuepuka vitendo vya rushwa kwa kutoa viwango halisi vya majengo ili kujijengea uaminifu wa kazi yao; https://youtu.be/o9lGqggg7Ms

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Prof Makame Mbarawa amesema serikali iko katika mkakati wa mazungumzo na serikali ya China kuboresha chuo cha Usafirishaji NIT; https://youtu.be/THNXKFjGNV0

SIMU.TV: Waziri Jenista Mhagama amewataka vijana wa kitanzania kujikita katika mafunzo ya ushonaji wa nguo ili kupunguza tatizo la ukosefu  wa ajira;https://youtu.be/iZwLxZwD9t4

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla, amesema kamwe hawezi kuwavumilia wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara zao sehemu zisizo rasmi;https://youtu.be/J93DKLsraxk

SIMU.TV: Kampuni ya uuzaji magari ya Nissan yalalamikia kupungua kwa mauzo nchini huku sababu kubwa ikitajwa ni adhima ya serikali ya kubana matumizi;https://youtu.be/HsHEiKiyY3E

SIMU.TV: Timu ya taifa ya kuogelea iliyokuwa nchini Brazil kushiriki mashindano ya Olimpiki imerejea nchini hii leo huku wakiahidi kufanya maajabu katika mashindano yajayo; https://youtu.be/xLBVGjf1GMc

SIMU.TV: Kikosi cha timu ya vijana Serengeti boys kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wa marudiano na timu ya vijana ya afrika ya kusini utakaopigwa uwanja wa Azam Complex Chamazi; https://youtu.be/-rNQ_J4ha7A

No comments: