Meneja wa Bank of Africa (BOA), tawi la Babati, Goodluck Mwasa akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa tawi hilo.
Meneja wa Bank of Africa (BOA), tawi la Babati, Goodluck Mwasa (kulia), akifafanua jambo kwa Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis Massawe. Wa pili kushoto ni mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Longino Kazimoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa, Ammishaddai Owusu-Amoah akitoa hotuba fupi kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la Babati mkoani Manyara.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Longino Kazimoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Ammishaddai Owusu-Amoah na Meneja wa Tawi jipya la Babati, Goodluck Mwasa.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Longino Kazimoto akikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa tawi jipya la Bank of Africa mjini Babati.
Waliokaa kutoka kushoto ni Samson Ntunga, akimuwakilisha Katibu Tawala (Manyara), Mkurugenzi Mtendaji wa wa Bank of Africa, Ammishaddai Owusu-Amoah akiwa na mgeni rasmi, Longino Kazimoto na RPC Franc
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, amesema maendeleo ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini hayawezi kuwa na mafanikio bila ya kuhusisha Sekta binafsi.
Bendera alitoa kauli hiyo, mwishoni mwa wiki katika sherehe za ufunguzi wa matawi mapya ya benki ya Tanzania yaliyofunguliwa, Babati mkoani Manyara.
Alisema Benki hiyo imedhamiria kupanua shughuli za kibenki nchini hasa katika kukuza uchumi wa watu wa Babati.
“Benki hii inakuja na mengi mapya katika Sekta ya Benki na kuleta huduma za kibenki karibu na wananchi wa Babati ikiungana na Benki zingine pamoja na kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania,”alisema Bendera na kuongeza “Niombe uongozi pamoja na wafanyakazi wote wa Benki ya Afrika kuhakikisha kwamba wateja wa tawi la Babati wanapata huduma za kipekee katika viwango vya kimataifa tukiweka pamoja na mahitaji ya wana Babati katika benki yenu. natumaini kuwa una wafanyakazi wenye sifa, uwezo na weledi wa kufanya kazi na hivyo unachohitaji sasa ni wateja,”alisema Bendera.
Bendera alisema Serikali inafanya kila iwezalo katika kuhakikisha huduma za kifedha zinamfikia kila mwanachi kwa urahisi na kwamba katika kuhakikisha hili linafanyika serikali itaboresha miundombinu hasa barabara, njia za mawasiliano na utengenezaji wa Sera zilizo stahiki na kupigana na umasikini.
Aliongeza kuwa Serikali itaendelea na jukumu lake la kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuhamasisha wawekezaji zaidi Nchini.
“ Pamoja na jitihada hizo bado kuna maeneo yanayohitaji kuboreshwa ili kujenga mazingira bora ya Sekta Binafsi kukua hasa suala la upatikanaji wa huduma za Kibenki Vijijini na katika Sekta ya Kilimo,”alisema Bendera.
No comments:
Post a Comment