Mgeni
rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo ,Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
waandamizi wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi pamoja na waendesha Baiskeli.
Mgeni
rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo ,Anastazia Wambura akiwa meza kuu kwa ajili ya zoezi la utoaji wa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.kulia kwake ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ,Asa Mwaipopo.
Mshindi wa kwanza katika Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Kanda ya ziwa yajulikanayo kama Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 ,Seni Konda akifurahia zawadi ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura.
Mshindi wa pili katika Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Kanda ya ziwa
yajulikanayo kama Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 ,Makoja Hamis akionesha zawadi ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi kikombe kwa mshindi wa tatu wa Mashindano hayo ya baiskeli, Hamis Clement.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akimvisha medali mshindi wa kwanza kwa upande wanawake wa mbio za baiskeli za Acacia tufanikiwe pamoja cycle Challange 2016,Martha Anthony.
Mshindi wa kwanza kwa upande wanawake wa mbio za baiskeli za Acacia tufanikiwe pamoja cycle Challange 2016,Martha Anthony akiwa amenyanyua juu kikombe mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa pili wa mashindano ya baiskeli ,Salma William .
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi zawadi ya kikombe na fedha kwa mshindi wa tatu wa mbio za baiskeli,Elizabeth Clement.
Washindi wa Mbio za Baiskeli kwa upande wa wanawake na wanaume katika mashindano ya Acacia tufanikiwe pamoja Cycle Challange 2016 wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Bingwa mara mbili wa mashindano ya Mbio hizo, Masunga Duba akipeana mkono na mgeni rasmi mara baada ya kuhitimisha mbio hizo akishika nafasi ya nne.
Mkuu wa kitengo cha biashara katika Mgodi wa Buzwagi,Jackson Kanumba akikabidhi zawadi kwa mshiriki wa mbio hizo Ashiraf.
Mshiriki Ashraf ambaye amekua akishiriki mashindano mbalimbali ya baiskeli ,akipongezwa na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa umma wa kampuni ya Madini ya Acacia,Necta Foya akikabidhi zawadi kwa mmoja wa washindi waliofanikiwa kuwa kati ya washiriki 30 bora.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa umma wa kampuni ya Madini ya Acacia,Necta Foya (katikati) pamoja na Afisa Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi,Magesa Magesa wakitoa maelekzo kwa mshereheshaji wa shughuli hiyo,Mc Kalinga.
Wasanii wa kikundi cha Ngoma wakitumbuiza katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa mbio za baiskeli.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.
FAINALI
ya mashindano ya mbio za baiskeli zijulikanazo kama “Acacia Tufanikiwe Pamoja
Cycle challange 2016 zinazoandaliwa na chama cha mchezo wa mbio za baiskeli
(CHABATA) na kudhaminiwa na kampuni ya kuchimba Madini ya Acacia zimemalizika mjini
Kahama huku mwendesha baiskeli Seni Konda akiweka rekodi ya kushinda mbio hizo
kwa kutumia saa 4:15:07 .
Konda
mkazi wa mkoa wa Shinyanga amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kuwashinda
wapinzani wake Makoja Hamis aliyemaliza nafasi ya pili na Hamis Clement
aliyemaliza nafasi ya tatu huku wakifuatiwa na waendesha baiskeli zaidi ya 150 walioshiriki
mbio hizo kutoka mikoa sita ya kanda ya ziwa.
Kwa
upande wa wanawake ,mwendesha baiskeli,Martha Anthony kutoka mkoani Mwanza
amefanikiwa kutetea ubingwa wake akimaliza wa kwanza huku akiwashinda
washindani wake,Salma William aliyeshika nafasi ya pili na Elizabeth Clement
aliyeshika nafasi ya tatu.
Mshindi
wa kwanza kwa upande wa wanaume ,Seni Konda amejinyakulia kitita cha sh Mil 1.5
,mshindi wa pili Makoja Hamis akijinyakulia kiasi cha sh Mil moja huku mshindi
wa tatu ,Hamis Clement akiambulia kiasi cha sh 700,000.
Upande
wan wanawake mshindi wa kwanza Martha Anhtony amejinyakulia kiasi cha sh Mil
1.2,mshindi wa pili Salma William akipata sh 800,000 huku mshindi wa tatu
,Elizabeth Clement akipata sh 600,000.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo mgeni rasmi naibu waziri wa
habari, utamaduni, Sanaa na michezo Anastazia Wambura amesema michezo ni ajira
na afya ambapo pia amewataka wachezaji kutotumia madawa ya kusisimua misuri kwa
kuwa kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za michezo na atakayebainika
atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha
Baiskeli cha Tanzania (CHABATA)
Jacx Mhagama alisema CHABATA na kampuni
ya madini ya ACACIA wamesaini mkataba wa udhamini wa mashindano hayo kwa muda wa miaka mitatu kuanzia 2014 mpaka
2016.
“Kipindi hiki cha miaka
mitatu kimekuwa na mengi kiutendaji na kimahusiano kwetu sote CHABATA na
ACACIA. lakini kwetu imekuwa ni kipindi chenye chenye changamoto zenye
kutukomaza na kutujenga. Hivyo tumevuna
tuliyoyategemea na ziada pia.”alisema Mhagama.
“ACACIA ni kampuni yenye
machimbo ya madini kwenye eneo hili la kanda ya Ziwa, lakini wameonyesha upendo
na uzalendo mkubwa hata kwa Taifa. Pamoja na kujishughulisha na michezo kwenye
eneo hili la kanda ya ziwa, wameenda juu Zaidi kufikia taifa kwa kuifadhili
timu yetu ya Taifa ya Baiskeli kwenye mashindano ya Ubingwa wa Afrika mwaka
jana 2015, yaliyofanyika huko Petermarizburg nchini Afrika ya Kusinu.”aliongeza
Mhagama.
No comments:
Post a Comment