Tuesday, July 19, 2016

WANANCHI WA KIJIJI CHA KISEGESE WILAYANI MKURANGA WAMEIOMBA SERIKALI IWAJENGEE BARABARA.

  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ametembelea shule ya msingi Kisegese,ambapo pia aliweza kuchangia sh.milioni moja katika uazishaji wake leo katika ziara ya kuwashukuru wananchi baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika 2015,leo Julai 18, 2016 katika Kijiji cha Kisegese wilaya Mkuranga mkoani Pwani.
 Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega ametembelea shule ya msingi Kisegese,ambapo pia aliweza kuchangia sh.milioni moja katika uazishaji wake leo katika ziara ya kuwashukuru wananchi baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika 2015,leo Julai 18, 2016 katika Kijiji cha Kisegese wilaya Mkuranga mkoani Pwani. kushoto kwake anayempa maelezo ni Diwani wa Kata ya Kisegese, Jumanne Mapande.
 Wananchi wa Kijiji cha Kisegese wilaya Mkuranga mkoani Pwani wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega.
 Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akiwasili Kijiji cha Kisegese wilaya Mkuranga mkoani Pwani.


Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akiwasili Kijiji cha Kisegese wilaya Mkuranga mkoani Pwani.

Na Mwandi wetu.
WANANCHI wa Kijiji cha Kisegese wilaya Mkuranga mkoani Pwani wameiomba Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya hiyo kufanya haraka ujenzi wa barabara kwani wamekuwa wakipata shida hata kufikia huduma za Jamii ikiwa pamoja na Zahanati.

Wananchi hao walitoa maombi hayo kijijini hapo leo mara baada ya Mbunge wa Jumbo hilo Abdallah Ulega kufanya ziara ya kuwashukuru baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.Akizungumza kwaniaba ya wananchi wake Mwenyekiti wakijiji hicho Jika Sultan alisema kuwa kwanza wanampongeza mbunge wao kwa kuweza kukumbuka kurudi kwao kwa lengo la kuwashukuru lakini kero kubwa wanayokutana nayo ni ukosefu wa miundombinu ya barabara.

"Barabara imekuwa ni changamoto kubwa katika kijiji chetu kama ulivyoona mh.mbunge nadhani hata wewe mwenyewe umeona na kwa bahati nzuri umeongozana na wataalamu mbalimbali kutoka halmashauri ya mkuranga.tunaomba muiangalie barabara hii."alisema Sultan

Aidha mbali na changamoto ya barabara pia hawana Zahanati kwani wanalazimika kusafiri umbali mrefu kutoka kijijini hapo hadi Mtamba kwa ajili ya kufuata huduma hiyo.

Akizungumzia elimu alisema Kata ya kisegese haina shule ya Sekondari hivyo wanaiomba halmashauri hiyo kushirikiana na wananchi ili kufanikisha ujezi wa shule hiyo.

Pia shule ambazo zipo hususani shule za msingi hakuna umeme 'wala maji hivyo wanaomba serikali kuweza kuangalia eneo hilo huku akitilia mkazo miundombinu ya barabara.

"Tunakuomba mh.Mbunge kuweza kutusaidia kutatua changamoto hizi na tunaamini kufika kwako ni faraja kwetu na hakuna shaka kwamba Kero hizi zitapata majibu."alisema msomaji wa risala kwa mbunge Pharles Masanyiwa.

Naye Diwani wa Kata hiyo jumanne Mapende akizungumza mbele ya Mbunge Ulega alisema kuwa Kata yake mbali na changamoto zingine lakini tatizo kubwa wanalokabiliana nalo wananchi wake ni barabara.

Alisema anampongeza mbunge kwani ameweza kuambatana na watalaam ili kujionea hali halisi ya barabara hiyo hivyo kusikia majibu juu ya barabara ya kizavala viazi kisegese na viazi Chamgoi kwani wametabika kwa muda mrefu.

Akitoa hotuba yake mbele ya wananchi wa kijiji cha Kisegese Mbunge Ulega alisema kwaza ameradhimika kurudi kijijini hapo ili kutoa shukrani zake na pia kama ahadi yake kwao yakuwa karibu na watu wake.

Alisema kuwa aliahadi kuwa karibu mno na wananchi hata kama akichaguliwa kuwa mbunge wa Jumbo hilo huku akiwahakikishia watashirikiana kwa karibu ikiwa pamoja na kukagua mambo mbalimbali ambayo alipanga kuyatekeleza.

Pia Ulega aliwaeleza wananchi hao kuwa katika ziara yake amelazimika kuja na watendaji na watumishi kutoka halmashauri ili kuhakikisha changamoto za watu hao zinamalizika huku akiwataka watumishi hao kutekekeza adhima ya Serikali kuwatumikia wananchi wake.

"Ndugu zangu Nataka niwakikishie kwamba serikali hii chini ya Rais Dkt.John Magufuli hakuna mchezo hivyo lazima tuchape kazi na Mimi kama Mbunge wenu nipo pamoja nami ,tutashirikiana kwa nguvu zote ili kuhakikisha kwa pamoja tunapata maendeleo."alisema Ulega

Aidha alisema kuwa katika kuonesha anatembea kwenye ahadi zake tayari amechangia sh.milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi huku akisisitiza kuendelea kufanya hivyo kadri pesa itakapokuwa inapatikana.

Akizungumzia bajeti ya serikali ya 2016/17 mbunge huku akipata maelekezo kutoka kwa Injia wa Halmashauri ya mkuranga zimetengwa sh.Milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa awali wa Barabara ya kizala ,viazi kisegese,na viazi chamgoli.

Mbali na kisegese pia Mbunge Ulega ametembelea pia kijiji cha Viazi kilichopondani ya Kata hiyo ya Kisegese.nakudai kuwa leo atatembelea Kata ya Pazuo.

No comments: