Thursday, July 7, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

SIMU.TV: Siku chache baada ya mamlaka ya udhibiti wa mafuta EWURA kutangaza bei mpya za mafuta, wakazi wa mkoani Mtwara wakosa mafuta kabisa;https://youtu.be/MlBh1CfRWZE

SIMU.TV: Waumini wa dini ya Kiislamu wilayani Urambo mkoani Tabora, wameaswa kuendelea na matendo mema licha ya kumalizika kwa mfungo wa ramadhani;https://youtu.be/Z5FVL-yc6jE

SIMU.TV: Wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya mifupa MOI, wamepewa chakula na matunda na waumini wa dini ya Kiislamu;https://youtu.be/COWBMiayAvs

SIMU.TV: Australia na Tanzania wamedhamiria kuimarisha mahusiano yao kiuchumi, huku serikali ya Tanzania ikisisitiza nguvu kubwa ya uwekezaji ielekezwe katika sekta ya kilimo;https://youtu.be/AP-Uo59V3fk

SIMU.TV: Benki ya CRDB imeendelea kuwasisitiza wananchi kufanya miamala yao kwa kutumia simu za kiganjani ili kupunguza vitendo vya uporaji na unyang’aji;https://youtu.be/H7G7qM73dcE

SIMU.TV: Pamoja na jitihada za kuimarisha miundombinu ya teknolojia ya ujenzi wa mkongo wa taifa, Tanzania bado iko nyuma katika matumizi ya TEHAMA kwa Afrika Mashariki; https://youtu.be/1Yplnpyx7Dg

SIMU.TV: Timu ya watanzania wanaoishi jimboni Maryland nchini Marekani, wametoa misaada ya kofia na miwani kwa watu wenye Ualbino walioko nchini Tanzania;https://youtu.be/3_EikxOyF_A

SIMU.TV: Watoto wa kiume na kike wanaoishi katika kituo cha kulelea wenye mazingira magumu wilayani Kisarawe manispaa ya Temeke, wanalazimika kutembea umbari mrefu kufuata masomo; https://youtu.be/EVh4jT8pDjI

SIMU.TV: Kamati ya maadili ya shirikisho  la mpira nchini TFF, limemfungia Jerry Murro kujihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili; https://youtu.be/6PBkrBkAMrA  

SIMU.TV: Muigizaji mkongwe kutoka India Akun Kapoor tayari ameshawasili nchini kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la kimataifa la filamu Zanzibar ;https://youtu.be/vTm2zQs9cuc

SIMU.TV: Maendeleo ya mchezo wa Gold nchini yatapatikana endapo watanzania watajitoa kushiriki ikiwa ni pamoja na wadau kudhamini mchezo huo;https://youtu.be/qotaCMQAn2k

SIMU.TV: Timu mbalimbali zimechuana leo katika bonanza la Jahazi soka kwa Maveteran  lililofanyika katika viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam; https://youtu.be/yO0fR8GGPdg

SIMU.TV: Ureno imefanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya mashindao ya Euro baada ya kuwafunga timu ya taifa ya Wales kwa jumla ya mabao 2-0;https://youtu.be/evKvTncABl4

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa majiji matano, manispaa, miji  na halmashauri zote za wilaya za Tanzania bara.https://youtu.be/nn_tz19R9kc

SIMU.TV: Rais amemteua Ndugu Deogratius Ndejembi kuwa mkuu wa wilaya ya Kongwa kuchukua nafasi ya Ndugu John Ernest Palingo aliyehamishiwa wilaya ya Mbozi.https://youtu.be/FOpWcTkgnP4

SIMU.TV: Viongozi wa dini ya kiislamu wamewataka waumini wa dini hiyo kuhakikisha watoto wanapata elimu itakayowawezesha kupambana na maisha.https://youtu.be/A3ADwfXGdME

SIMU.TV: Baraza kuu la taasisi za kiislamu mkoani Katavi limeshauriwa kuendelea kuwaasa waumini wake kuendelea kudumisha amani ya nchi. https://youtu.be/2vtShtdrR4M

SIMU.TV: Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi leo katika kilele cha maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba. https://youtu.be/H7-J66rNgt0

SIMU.TV: Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge Jenista Mhagama ametoa wito kwa kampuni zinazofanya kazi nchini kuhakikisha wanalipa mafao kwenye mifuko ya jamii. https://youtu.be/mpHebHrbKso

SIMU.TV: Wakala wa huduma za misitu mkoani kanda ya ziwa wamefafanua kodi ya serikali ya tozo ya shilingi 425000 baada ya kambi za wavuvi katika Visiwa vya Kome na Maisome kuteketea kwa moto. https://youtu.be/NpUi-DVSGAk

SIMU.TV: Mkoa wa Songwe umeanza kutekeleza agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za waalimu na matundu ya vyoo. https://youtu.be/__7kajg1Nkg

SIMU.TV: Viongozi wa ngazi mbalimbali katika jamii wameshauriwa kutoa elimu ya afya kwa jamii ili iweze kujikinga na maradhi mbalimbali. https://youtu.be/yo1sccDoulQ

SIMU.TV: Ikiwa imebaki siku chache uongozi wa CCM kumchagua mwenyekiti wake, uongozi wa CCM mkoani Iringa umelaani tamko la vijana wa CHADEMA la kutaka kwenda kuvuruga mkutano huo. https://youtu.be/zKhetKvRYBA

SIMU.TV: Mamia ya wakazi mkoani Arusha wamejitokeza katika maziko ya aliyekua mbunge wa jimbo la Kilindi Beatrice Shelukindo. https://youtu.be/py1kF66Sv1g

SIMU.TV: Kamati ya maadili ya shirikisho la soka nchini imemfungia msemaji wa klabu ya Yanga Jery Muro kujihusisha na soka kwa mwaka mmoja. https://youtu.be/r__uOImaGbo

SIMU.TV: Klabu ya Azam imeanza mazoezi ya kujifua kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara. https://youtu.be/3B32cH3i-wA

SIMU.TV: Klabu ya Mtibwa Sukari imesema bado ipo kwenye mawindo ya kupata mbadala wa wachezaji wake waliosajiliwa kwenye klabu za Simba na Yanga.https://youtu.be/VdrBqBp8DhI

SIMU.TV: Licha ya Ureno kuonekana timu inayopita kwa bahati sana katika mashindano ya EURO lakini imekua timu ya kwanza kutinga fainali za michuano hiyo baada ya kuitoa Wales. https://youtu.be/IAEEMgkNA14

No comments: