Saturday, July 16, 2016

IGP MANGU AWAVISHA NISHANI IGP WASTAAFU NA MAOFISA WENGINE WA POLISI

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu akikagua gwaride jana katika chuo cha taaluma ya Polisi Dar es Salaam wakati wa sherehe ya kuwavisha nishani IGP mstaafu Omari mahita na IGP mstaafu Saidi Mwema pamoja na maafisa wengine wa Polisi, nishani ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika. IGP Mangu amewavisha nishani kwa niaba ya Mwenyekiti wa shirikisho hilo wa sasa. Tukio lilifanyika jana katika chuo cha taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu akimvisha nishani IGP mstaafu Omari Mahita, nishani ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa kuwa IGP wa kwanza Tanzania kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo na kuliletea sifa Jeshi la Polisi Tanzania kimataifa. IGP Mangu amemvisha nishani kwa niaba ya Mwenyekiti wa shirikisho hilo wa sasa. Tukio lilifanyika jana katika chuo cha taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu akimvisha nishani IGP mstaafu Saidi Mwema, nishani ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa kuwahi kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo na kuliletea sifa Jeshi la Polisi Tanzania kimataifa. IGP Mangu amemvisha nishani kwa niaba ya mwenyekiti wa shirikisho hilo wa sasa. Tukio lilifanyika jana katika chuo cha taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu akimpongeza IGP mstaafu Omari Mahita, baada ya kumvisha nishani ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa kuwa IGP wa kwanza Tanzania kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo na kuliletea sifa Jeshi la Polisi Tanzania kimataifa. IGP Mangu amemvisha nishani kwa niaba ya mwenyekiti wa shirikisho hilo wa sasa. Tukio lilifanyika jana katika chuo cha taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu akimpongeza IGP mstaafu Saidi Mwema, baada ya kumvisha nishani ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa kuwahi kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo na kuliletea sifa Jeshi la Polisi Tanzania kimataifa. IGP Mangu amemvisha nishani kwa niaba ya mwenyekiti wa shirikisho hilo wa sasa. Tukio lilifanyika jana katika chuo cha taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Ernest Jumbe Mangu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Jeshi la Polisi wastaafu, IGP Omari Mahita (kushoto) na IGP Saidi Mwema. IGP mstaafu Mahita na IGP mstaafu Saidi Mwema walivishwa nishani jana katika Chuo cha taaluma ya Polisi Dar es Salaam, nishani ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa kuwahi kuwa mwenyeviti wa shirikisho hilo na kuliletea sifa Jeshi la Polisi Tanzania kimataifa. Nishani walivishwa na IGP Mangu kwa niaba ya mwenyekiti wa shirikisho hilo wa sasa.Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

No comments: