Baadhi
ya vikundi mbalimbali vikisubiri kuanza mbio za Tulia Marathon KM 5
zikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kusaidia watoto Yatima na waishio
katika Mazingira Magumu,ambapo baada ya mbio hizo walikwenda kutoa
msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha Watoto Yatima kiitwacho
kijiji cha Matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.Wakati wa
kutoa msaada huo Dkt Tulia alisema kuwa ni vvema kila Mkoa vikawa na
vikundi mbalimbali kikiwemo cha Wazalendo wakafanya shughuli za Kijamii
kusaidia makundi mbalimbali.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson (wa
tatu kulia),akiwa ameongoza na Wabunge mbalimbali vikiwemo na vikundi
vya kuhamasisha mbio hizo zilizoanzia geti la Bunge na baadae kuishi
katika viwanja vya Vya Nyerere Skwea mjini Dodoma.
Baadhi
ya Wabunge wakishiriki mbio za Tulia Marathon KM 5 mapema leo,ambapo
mbio hizo zilikomea katika viwanja vya Nyerere Skwea
Vikundi mbalimbali vikiunga mkono mbio za Tulia Marathon KM 5 mapema leo asubuhi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia
Ackson (wa nne kulia),akiongoza mbio za Tulia Marathon KM 5 akiwa sambamba na baadhi ya Wabunge mbalimbali vikiwemo na
vikundi vya kuhamasisha mbio hizo zilizoanzia geti la Bunge na baadae
kuishi katika viwanja vya Nyerere Skwea mjini Dodoma.Dkt Tulia na washiriki wa mbio hizo. Baada ya mbio hizo walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika
kituo cha Watoto Yatima kiitwacho kijiji cha Matumaini kilichopo nje
kidogo ya mji wa Dodoma.Wakati wa kutoa msaada huo Dkt Tulia alisema
kuwa ni vvema kila Mkoa vikawa na vikundi mbalimbali kikiwemo cha
Wazalendo wakafanya shughuli za Kijamii kusaidia makundi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment