Tuesday, July 12, 2016

DROO YA 7 YA TUSKER FANYA KWELI UWINI YATOA MAMILIONEA WENGINE 10Mmoja wa washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini, Mr. Geofrey Manangwa kutoka Tanga akifanya maandalizi ya duka lake jipya mara baada ya kupata Milioni moja kutoka Tusker iliyomsaidia kuongezea mtaji wa kufungua duka la nafaka.

Watanzania waendelea kuwa na muamko zaidi huku promosheni ikielekea ukingoni.

 
 Wiki iliyopita imekua ni wiki yenye shamrashara nyingi za sikukuu na ikamalizika kwa kufanyika kwa droo ya saba ya promosheni ya ‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ iliyofanyika katika studio za ITV ambapo washindi wengine kumi walitangazwa huku wakiibuka na Tsh Milioni moja kila mmoja. 

Droo hiyo iliyoshuhudiwa na waangalizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, wakaguzi wa nje na washirika wengine, inafanya idadi ya washindi kufikia washindi 80 kutoka mikoa tofauti hapa nchini walioshinda kwenye droo za kila ijumaa ya kila wiki na tayari wameshapokea pesa zao.

“Tayari tumeshatoa Milioni 80 kwa washindi wetu mpaka sasa lakini pia kuna zawadi kibao ambazo wateja wetu wanajishindia ikiwa ni pamoja na bia za bure, kofia na t-shirts wanazopata baa kila mwisho wa wiki ijumaa na jumamosi tunapoendesha shuguli zetu za mauzo sokoni.

 Nawakumbusha wateja wetu waendelee kushiriki mara nyingi kadiri wawezavyo kwani kushiriki mara nyingi kunampa nafasi nyingi zaidi za kushinda Mamilioni ya pesa” alisema Afisa Mipango na Uratibu kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti - Lulu John Mduma. Pia aliongeza kuwa “siku zote kitu kizuri hakidumu muda mrefu tunategemea kumpata mshindi wetu wa 100 wiki mbili zijazo”.

Naye Meneja wa Bia ya Tusker - Jasper Maston Migambile akizungumza na wanahabari mara baada ya droo hiyo alisema, “Droo ya leo imeongeza muamko zaidi kwani kilichonifurahisha zaidi ni kushuhudia mteja mmoja Bwana Gastor Mjakonde kutoka Pwani kushinda mara mbili na kuibuka na Milioni mbili, hii ni bahati ya kipekee lakini inaweza kutokea kwa mtu mwingine kwa droo zinazofuata,”

Aliongeza kwa kusema kuwa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini imewapa nafasi kugusa na kubadilisha maisha ya wengi kama walivyotoa ushuhuda baadhi ya washindi walioshinda tangu kuanza kwa promosheni hiyo. “Tunajivunia kuona washindi wetu wengi wamekeza pesa walizoshinda katika matumizi yenye manufaa kama kulipia ada za shule, kuongezea mtaji katika biashara zao, kuanzisha biashara, kumalizia ujenzi, kulipia kodi ya pango nakadhalika. Haja yetu kubwa nikuona wateja wetu kushuhudia namna nzuri ya matumizi ya pesa walizojishindia na kubadili hali zao za kimaisha kutoka hatua moja hadi nyingine.” Alisema Jasper.

Kuna mshindi mmoja kutoka Tanga Geofrey Manangwa ambaye ni mtumishi wa jeshi la polisi Tanzania na pia ni msimamizi wa biashara ya familia. Katika biashara yake ya sasa pia alikua na mipango ya kufungua biashara nyingine ya duka la kuuza nafaka lakini bado hakuwa na mtaji wa kutosha. 

“Nilikua na mipango ya kufungua duka la nafaka lakini nilikua bado najipanga taratibu, shukrani sana kwa Tusker sasa naweza kufungua duka langu muda wowote kwani tayari Milioni moja niliyoipata kutoka kwao imeniharakishia taratibu zote na kunipa wepesi wakumalizia maandalizi ya duka langu la nafaka,” alisema Bwana Geofrey.

Alishauri watanzania kutokuzarau kiasi chochote cha pesa kikubwa ni kuwa na mikakati na mipango mizuri kama ilivyokua kwake kwa kupata Milioni moja na matokeo yake yataonekana hivi karibuni. “Kikubwa kinachohitajika ni kuwa na mipango mikakati na si kukurupuka kufanya vitu tu, kwa kiasi chochote kile cha pesa unachopata,” alihitimisha Geofrey.

Washindi wa droo ya 7 ya Tusker Fanya Kweli Uwini ni:- Emmanuel Kitandu kutoka Dar es Salaam, Gastor Mjakonde ambaye ameshinda Tshs 2M na Martin Daffa kutoka Pwani, Peter Kaaya kutoka Arusha, Bakari Nasoro kutoka Moshi, David Assenga kutoka Morogoro, Geofrey Ng’amilo kutoka Iringa, Mau Charles kutoka Mara na Sabatho Ezeliel kutoka Shinyanga.

‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ ni promosheni iliyoanza takribani wiki saba zilizopita mikoa yote nchini. Wiki mbili tu zimesalia kukamilisha washindi 100 wa promosheni hiyo.

No comments: