Tuesday, July 12, 2016

CHAMA CHA WAAJIRI (ATE) CHAZINDUA PROGRAM YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO

 Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka akizungumza wakati wa uzinduzi wa program ya Mwanamke wa Wakati Ujao inayolenga kuboresha ufanisi utakaowawezesha kumudu nafasi za uongozi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. 
 Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka (kulia), akishikana mikono Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia), katika hafla ya uzinduzi wa program ya Mwanamke wa Wakati Ujao jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi za Jamii (SSRA), Irene Isaka.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi za Jamii (SSRA), Irene Isaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa program ya Mwanamke wa Wakati Ujao jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Laurean Bwanakunu akizungumza na washiriki katika hafla hiyo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akizungumza katika uzinduzi huo.
 Meneja Vipaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Lilian Makau Galinoma akizungumza na washiriki wa program hiyo ilipozinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simba Cement, Reinhardt Swart (kushoto), akifurahi na baadhi ya washiriki na waandaaji wa uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka pamoja na baadhi ya wawakilishi wa makapuni yanayosapoti program ya Mwanamke wa Wakati Ujao (walioketi), wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya washiriki wa program hiyo.
 Baadhi ya washiriki wa program hiyo wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa program ya Mwanamke wa Wakati Ujao jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya washiriki wa program ya Mwanamke wa Wakati Ujao (Female Future) wakihudhuria hafla ya uzinduzi jijini Dar es Salaam leo. 

No comments: