Friday, July 22, 2016

BENKI YA CRDB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 100 - KIGOMA

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kasulu mkoani Kigoma Paul Chacha akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya Kakonko madawati 100 yenye thamani ya Sh. Mil 5 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa madawati katika Shule za Msingi wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko mkoani Kigoma Lusubilo Mwakabibi (aliyesimama kati kati) akizungumza muda mfupi kabla ya benki ya CRDB haijakabidhi madawati 100 yenye thamani ya Sh. Mil 5 kwa ajili ya shule za msingi wilayani humo. 
Mkuu wa wilaya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza kabla hajapokea madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule za Msingi wilayani humo. 
Mkuu wa wilaya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala (kulia) akipokea kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kasulu mkoani Kigoma moja ya madawati 100 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za Msingi wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagaa (kulia) akipokea sehemu ya msaada wa madawati 100 kutoka kwa Meneja wa CRDB Tawi la Kasuu, Paul Chacha. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Hamashauri ya Wilaya ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi (katikati) na ofisa wa CRDB.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (walioka kulia) akiwa na Meneja wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (katikati) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi. Kushoto waliosimama ni Katibu Tawala wa Kakonko, Zainab Mbunda. 
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (kulia) akimshukuru Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha baada ya kupokea msaada wa madawati 100 kwa ajili ya Shule za Msingi Wilayani humo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala (katikati) akiwa na Meneja wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi (kushoto) na Katibu Tawala wa Kakonko, Zainab Mbunda.

No comments: