Kikundi cha wajasirimali wanawake kutoka Tanzania (Tanzania Saccos for Women Enterprenuers) kinachoongozwa na Bi. Anna Matinde Mkurugenzi wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania waliwasili nchini Comoro kwa ajili ya ziara ya siku mbili. Lengo la ziara hiyo ni kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa za kutoka Tanzania, pamoja na kukutana na wajasiriamali wa Komoro ili kuweza kubadilishana taarifa juu ya fursa mbalimbali za biashara kati ya Tanzania na Komoro.
Wajasirimali hao waliwasili nchini Komoro tarehe 13 Juni 2016 na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka F. Kilumanga. Wakati wakiwa nchini Komoro, wajumbe walipata fursa ya kukutana na wajumbe kutoka sekta binafsi ya Komoro pamoja na wa Tanzania waishio Komoro (Diaspora). Ujumbe huo ulifurahishwa sana na fursa za biashara zilizopo Komoro ambapo walielezea kuwa wapo tayari kushirikiana na Wakomoro katika kuleta bidhaa mbalimbali katika soko la Komoro.
Aidha, wajumbe walipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Watanzania waishio Komoro (TADICO). Katika majadiliano yao, wajumbe waliweza kushaurina juu ya mikakati ya kufanya biashara nchini Komoro, ambapo Bi. Matinde aliwaaelezea wanadiaspora wasisahu pia kuekeza nyumbani kwani nako kuna fursa nyingi hivyo ni muhimu kwa wanadiaspora kuangalia namna gani na wao wanaweza kunufaika na fursa hizo.
Wajumbe pia walipata fursa ya kuonyesha na kutangaza biashara zao kwa wafanyabiashara wa Komoro ambapo walionyeshwa kuvutiwa sana na bidhaa za kutoka Tanzania. Ikumbukwe kwamba Komoro ni nchi ambayo hutegemea kwa kiasi kikubwa bidhaa zake kutoka nje. Biashara kati ya Tanzania na Komoro imekuwa ikikuwa siku hadi siku hata hivyo, bado kuna mahitaji makubwa ya bidhaa za chakula na imeonekana kuwa Tanzania ndio nchi iliyo katika nafasi nzuri kukidhi mahitaji hayo, kutokana na ukaribu wa nchi hizo kijiografia na kimila.
Sambamba na hilo, kikundi cha wajasirimali wanawake kutoka Tanzania wanatarajia kutiliana saini mkataba wa ushirikiano (Memorandum of Understanding) baina yao na vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wa Komoro. Katika maelezo yake, Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Mhe. Chabaka Kilumanga alieleza kuwa huu ndio wakati muafaka wa vikundi hivyo vikaanza kufanya kazi kwa pamoja na kujuana ili kuweza kuboresha na kukuza wigo wa biashara kati ya Tanzania na Komoro. Alieleza pia kuwa ubalozi utaaendelea kushirikiana na wanadiaspora iwapo watapendelea kufanya kazi kwa pamoja na wajasirimali hao.
Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Chabaka Kilumanga akichangia mada katika warsha hiyo.
Bi. Anna Matinde, Mkurugenzi Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania.
Kikundi cha Wajasiriamali wanawake kutoka Tanzania wakiendelea kusikiliza mada.
Mkuu wa Utawala na Fdha Ubalizi wa Tanzania Komoro Bw.Mudrick Soragha alievaa tai nyekundu akikaribisha wageni.
Wadua wakilendelea kuangalia bidhaa kutoka Tanzania, katika ofisi za ubalozi, Moroni.
wafanyakazi wa Ubalozi katia picha ya pamoja na kikundi cha wajasiriamali wanawake kutoka Tanzania.
Wafanyakazi wa Ubalozi katika picha ya pamoja na wana Diaspora wa Komoro.
wajasiriamali wa Komoro wakiangalia bidhaa kutoka Tanzania.
Wajumbe kutoka Sekta Binafisi Komoro wakisikiliza kwa umakini mada.
No comments:
Post a Comment