Wednesday, June 15, 2016

JUKWAA LA MTANDAO UBUNIFU WA KITEKNOLOJIA LA UBER LAZINDUA USAFIRI WA UBER JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

 Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa jukwaa la mtandao ubunifu wa kiteknolojia la Uber.
Baadhi ya waanzilishi na wadau usafiri wa Uber wakiwa katika uzinduzi usafiri wa uber  jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wakiwa katika uzinduzi wa usafiri wa uber jijini Dar es Salaam leo.

JUKWAA la mtandao ubunifu wa kiteknolojia la Uber lazindua  usafiri wa Uber  jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la urahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits  amesema kuwa jukwaa la ubunifu wa kiteknolojia, Dar es Salaam inaungana na orodha ya vituo maarufu vya usafiri barani Afrika, mafanikio ya Uber katika nchi nyingi imeshazinduliwa na kuwa na mafanikio makubwa.

“Tunajivunia kuzindua Uber nchini Tanzania katika muda ambao uchumi wake unakua. Wakati miundo mbinu ya Dar es Salaam ikiwezeshwa kuwa ya viwanda, hivyo huongezeka kwa mahitaji ya usafiri nafuu, rahisi na wa kuaminika.”Amesema Lits.

Lits amesema kuwa kwa kutumia usafiri huo 
wasafiri watasafiri kwa muda muafaka ukiwa na program ya maombi ya usafiri(Application), kwa kubonyeza tu kitufe ambacho kitatoa taarifa kwa dereva aliyepo karibu pia amesema kuwa Uber husaidia watu kupata usafiri kwa kubonyeza tu kitufe pia hakuna kusubiri barabarani au kutembea maeneo jirani usiyoyajua kwa ajili kutafuta basi. 

    Amesema kuwa hakuna haja kusimamisha gari mtaani au kuwa nje kusubiri usafiri. Kwa usalama zaidi utaweza kutumia App ya Uber mahali ulipo ukisubiri gari ifike. Hii ikimaanisha hakuna haja ya kusimama barabarani kusubiri taksi au kuhangaika kutafuta kituo cha basi kilicho karibu muda wa usiku.   

    Safari hazina kificho mara dereva anapokubali ombia lako, unaona jina lake la kwanza, picha na namba ya gari yake. Pia unaweza kuangalia kama kuna abiria wengine waliofurahia huduma yake. Kwa kuongezea, dereva anaweza kuona jina lako la kwanza na alama ulizompa. Unaweza kuwasiliana na dereva, naye pia akawasiliana nawe-kupitia hii App kama kuna mkanganyiko wowote kuhusu muda wa kukuchukua. 

“Uber ni sehemu ya mageuzi makubwa duniani katika Nyanja ya usafirishaji. Dar es Salaam ipo juu, inazizima, mji unaokuwa ukiwa na vijana mahiri wenye nguvu ya kufanya kazi ambao wapo tayari kutukaribisha na kusapoti huduma yetu. Pamoja, kwa ushirikiano na mipango ya usafiri iliyopo jijini Dar es Salaam tunaweza kubadilisha sura ya usaifiri wa mjini kunufaisha abiria. Tuna furaha isiyo na kifani kwa uzinduzi huu.”amesema.

No comments: