Monday, June 20, 2016

WASHINDI WA KAMPENI YA "Shinda na TemboCard" WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO NA BENKI YA CRDB

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafala ya kukabidhi zawadi kwa kwa washindi wa Kampeni ya "Shinda na TemboCard" iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akitoa hotuba yake wakati wa hafala ya kukabidhi zawadi kwa kwa washindi wa Kampeni ya "Shinda na TemboCard" iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Kampeni ya "Shinda na TemboCard" akiwa katikapicha ya pamoja na mshindi aliyejishindia simu aina ya iphone 6, Barbara Hassan (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia).
Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto), akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege ya kwenda Dubai mshindi wa kwanza wa Kampeni ya "Shinda na TemboCard" kwa upande wa wateja, Ismail Jimroger wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB  wakiwa katika hafla hiyo.

 Baadhi ya wakurugenzi na Mameneja wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.

No comments: