Monday, June 20, 2016

BUNGE LAPITISHA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA KISHINDO MJINI DODOMA

Bunge limepitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya serikali yenye malengo ya kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Triln 29.54, ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zitatumika kwaajili ya miradi ya maendeleo na kiasi kilichobaki kitatumika kwa matumizi ya kawaida.
Idadi ya wabunge walioshiriki kupiga kura walikuwa 251 na wote wamepiga kura za ndiyo na kuipitisha bajeti Kuu hiyo kwa asilimia 100 pamoja na kupitisha sheria ya fedha kwa mwaka 2016/2017.
Picha zote zinahusu matukio yaliyotokea ndani na nje ya viunga vya Bunge mjini Dodoma, ikiwemo wabunge na baadhi ya wananchi waliohudhuria uhitimishaji wa Bajeti hiyo, wakimpongeza Waziri na watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kufanikisha kazi kubwa ya kuandaa bajeti hiyo.
Picha zote na WFM

Imetolewa na 
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

No comments: