Sunday, June 5, 2016

VYANZO VYA MAJI VYATAKIWA VILINDWE: SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Wilson Nkambaku aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Msingi Kiranyi.Ameagiza wananchi wote walijenga kwenye eneo lilitengwa kwaajili ya chanzo cha maji wabomoe wenyewe. 
Mtendaji Mkuu wa Mamkala ya Mji Mdogo wa Ngaramtoni,Sophia Shoko akizungumza jambo katika maadhimisho hayo. 
Diwani wa Kata ya Kiranyi ,halmashauri ya wilaya Arusha DC,John Seneu alikiwataka wananchi kutii sheria ili kulinda vyanzo vya maji. 
Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Wilson Nkambaku(katikati) aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha akifurahia jambo na Katibu Tawala mkoa(RAS),Richard Kwitega(kulia) kushoto Katibu Tawala Msaidizi huduma za Afya,Hargeney Chitukulo. 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Serikali ya mchepuo wa Kiingereza ya Arusha School wakiimba Shairi lao lenye kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kupanda miti. 
Baadhi ya viongozi kutoka halmashauri ya Arusha DC wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa wilaya. 
Baadhi ya viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha wadau wa taasisi binafsi na wananchi kwa pamoja wameshiriki kikamilifu Siku ya mazingira duniani. 
Baadhi ya mabalozi wa taasisi ya vijana wa Umoja wa Mataifa(UN)walioshiriki maadhimisho hayo katika Shule ya Msingi Kiranyi. 
Katibu Tawala(RAS)mkoa wa Arusha,Richard Kwitega akipanda mti katika maadhimisho ya siku ya mazingira leo. 
Mrembo Morine Ayub Mollel ambaye ameshinda taji la Miss Arusha akipanda mti kwenye bustani ya Shule ya Msingi Kiranyi. 

No comments: