Friday, June 24, 2016

UZINDUZI WA MFUMO WA MAWASILIANO WA KUBORESHA HUDUMA ZA RUFAA KWA MAMA NA MTOTO.

RUFAA  YA MAMA NA MTOTO KUTOLEWA KWA  HUDUMA  YA SIMU.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi amesema kuwa mfumo wa mawasiliano wa kuboresha  huduma ya Rufaa ya mama na mtoto kutasaidia akina mama na watoto wachanga huduma bora na matibabu wanayohitaji katika hospitali za rufaa.

Mushi ameyasema hayo  leo wakati Uzinduzi wa mfumo wa mawasiliano wa kuboresha  huduma ya Rufaa ya mama na mtoto , amesema kufanya mawasiliano ni njia ambayo inafanya  mgonjwa kupata huduma bora.
Amesema kuwa huduma hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam, imefika kwa muda mwafaka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu hivyo hata huduma zinatakiwa kuboreshwa.

Aidha amesema kuwa matumizi ya simu kwa vituo vya afya 127 vitaleta matokeo chanya na kuwa chachu kwa vituo vitakavyofuata kuendesha huduma hiyo itaweza ku huduma ya mama na mtoto.

Naye Meneja Mradi wa CCBRT, Brenda D’mello amesema kuwa Kamati ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam , ikishiriakiana na CCBRT  wanapambana na tatizo hafifu  kati ya zahanati  vituo vya afya  na Hospitali.

Amesema kuwa na mawasiliano hafifu husababisha rufaa ya wagonjwa  usio na mpangilio na ucheleweshwaji wa huduma na matibabu.
Brenda amesemavituo 23 na magari ya wagonjwa saba (7) yataunganishwa na mfumo wa simu  pamoja na ofisi za waganga wakuu wa wilaya na matabibu wa wa timu ya afya  ya mkoa.  
 Muuguzi akitoa mfano wa utoaji wa huduma kwa mama kwajia ya mfumo wa mawasiliano.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika uzinduzi wa Mpango wa mfumo wa mawasiliano kuboresha huduma za Rufaa kwa mama na mtoto. Akitoa simu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Aziz Msuya simu hiyo kwaajili ya kuboresha huduma hiyo.

 Watendaji waliokabidhiwa simu  maalum za mawasiliano kwaajili ya kutoa huduma za dhalula kwa mama na mtoto.
Baadhi ya wananchi waliohudhulia katika uzinduzi huo.

No comments: