Friday, June 24, 2016

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri 17 – Serengeti Boys, watembelea Airtel

Timu ya vijana chini ya umri 17 – Serengeti Boys, leo wamefanya ziara katika kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, ambao ni wadhamini wa michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars huku wakijiandaa na mechi ya Kimataifa ya kufuzu kucheza fainali za Afcon 2017 itakayochezwa jijini Dar es Salaam Jumapilihii.

Timu hiyo inajumulisha wachezaji kumi waliochunguliwa kutoka katika michuano iliyopita ya Airtel Rising Stars ambayo ilizinduliwa 2011 ikijumuisha mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mkurungenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya alisema kampuni inajivunia jinsi michuano ya Airtel Rising Stars ilivyowapa vijana fursa ya kuonyesha vipaji vyao vya soka na kupata nafasi ya kuchanguliwa kuchezea timu ya Taifa ya vijana.

Airtel Tanzania inayo furaha ya kupewa nafasi ya kudhamini mpira Tanzania kupitia michuano ya vijana ya kila mwaka ya Airtel Rising Stars. Michuano hii ni moja ya mipango yetu ya kuwapa fursa vijana kupitia kucheza mpira. Tunashukuru mpaka sasa hivi michuano hii imeweza kutoa wachezaji kumi ambapo wanachezea timu yetu ya taifa ya vijana – Serengeti Boys.

Wachezaji hao ni Ramadhan Awamu (Golikipa), Shabaan Zuberi, Cyprian Benedict na Ally Ng’anzi (Viungo), Mohammed Abdallah, Gadaffi Ramadhan na Nickson Clement (Mabeki), Mohammed Abdallah, Dickson Job,Muhsim Malama na Yohana Oscar (Washambuliaji).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya soka la vijana kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Ayoub Nyenzi alisema ili timu ya Taifa iweze kupata Mafanikio ni lazima kuwekeza kwenye miradi mbali mbali ya kukuza soka la vijana huku akitoa Shukrani kwa kampuni ya Airtel kuendeleza miradi huo kupitia Airtel Rising Stars.

Huu ni mwaka wa sita mfululizo wa michuano hii ya Airtel Rising Stars. TFF inatoa pongezi kwa Airtel kwa udhamini huu ambao umeweza kuwapa vijana wengi fursa ya kutambua uwezo wao, alisema Nyenzi.

Michuano wa Airtel Rising Stars awamu ya sita itazinduliwa Jumapili ya Juni 26 huku Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiwa mngeni rasmi. Uzinduzi huo pia utahudhuriwa na wadau wengine wa soka nchini wakimemo viongozi wa klabu, TFF, wachezaji wa zamani wa Airtel Rising Stars na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo wa soka la vijana Ayou Nyenzi akiongea na wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka U-17 Serengeti Boys wakati timu hiyo ilipotembelea Airtel Makao makuu jijini Dar es Salaam Juni 24, 2016.
Kocha wa Serengeti Boys Bakari Shime akiongea na wachezaji wakati timu hiyo ilipotembelea Airtel Makao makuu jijini Dar es Salaam Juni 24, 2016.
Mkurugenzi wa ufundi wa kamati ya maendeleo ya soka la vijana Kim Poulsen akiongea na wachezaji wa Serengeti Boys wakati timu hiyo ilipotembelea Airtel Makao makuu jijini Dar es Salaam Juni 24, 2016.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akiwapungia mkono wachezaji wa Serengeti Boys wakati timu hiyo ilipotembelea Airtel Makao makuu jijini Dar es Salaam Juni 24, 2016.
Mmoja kati ya wachezaji wa Serengeti Boys akiongea wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel makao makuu.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Serengeti boya ambao wametokana na program ya Airtel Rising Stars.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano na Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo wa soka la vijana Ayou Nyenzi (katika) wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti boys pamoja na viongozi wao wakati walipotembelea ofisi za Airtel Makao Makuu Morocco jijini Dar es salaam.

No comments: