Friday, June 24, 2016

TAASISI YA HASSAN MAAJAR TRUST YATOA MSAADA WA VITU VYA KUSOMEA KWA SHULE MBILI MKOANI MTWARA

 Taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa mara nyingine tena, wamefika mkoa wa Mtwara, kukabidhi kona za kusomea (Reading Corners) katika shule mbili, Lilungu na Nanguruwe. Jumla ya vitu walivyokabidhi ni madawati 60, makabati ya vitabu 4, vitabu 181, chati za mfano, herufi, hisabati pamoja na vifaa vya sanaa kama rangi za kuchorea, na kadhalika.
Mchango huu ni sehemu ya mradi wa DAWATI KWA KILA MTOTO (A Desk For Every Child) ambao umedhaminiwa na Shirika la marekani 'We are the world kids kama sehemu ya mpango wao wa kimataifa kujenga na kuanzisha maktaba na kona za kusomea kwa ajili ya shule za msingi na sekondari katika afrika na mashariki mwa Asia.'
 Mgeni wa heshima katika sherehe hii ni Mh. Halima Dendego -Mkuu wa Mkoa Mtwara, akiongozana na Mh.Fatuma Ally - Mkuu wa Wilaya Mtwara.
Sherehe hii ilifanyika katika shule ya msingi Lilungu (Mikindani).

No comments: