Thursday, June 23, 2016

KAMPUNI YA TOMONI FARMS LIMITED YAFUNGUA DUKA NA MGAHAWA WA KISASA WA MAZAO YA KILIMO DAR ES SALAAM

Kampuni ya Tomoni Farms Limited, inayomilikiwa na wazawa, wakijishughulisha na Kilimo cha umwagiliaji cha mazao ya Matunda na Mbogamboga, wamefungua duka na Mgahawa wa Kisasa kwa ajili ya uuzaji wa mazao yao katika hali ya usafi na usalama wa hali ya juu uliopo eneo la jirani na Victoria, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Jijini Dar Es Salaam, wakati wa utambulisho wa duka hilo na shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ya Tomoni Farms Limited, Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni hiyo Bwana Franklin Bagalla ameeleza kuwa, wameamua kuwasogezea watanzania bidhaa bora za kilimo ambazo watazipata moja kwa moja kupitia duka lao hilo na watajiona kama wapo shambani ama bustanini kwa namna ya uwekezaji wao walivyoweza kuuandaa ikiwemo mazingira safi na utunzaji wa kisasa kutoka shambani hadi kumfikia mlaji.
“Baada ya kuwekeza kwa miaka mine katika kilimo cha Matunda na Mboga mboga kwa kutumia teknolojia ya umwagiliaji, huku tukiwa na uhakika wa kutoa mazao Mwaka mzima, sasa tumewekeza katika miundo mbinu ya kuhakikisha mazao yetu yanawafikia walaji yakiwa katika hali ya usafi na usalama. Hivyo kupitia katika duka letu hili la kisasa hapa Dar es Salaam linatoa fursa kwa wananchi kujipatia bidhaa za kila aina na watazipata kwa hali ile ile kama zipo shambani na tunawakaribisha sana” alieleza Bwana Bagalla.
Aliongeza kuwa, Mazao yote yanavunwa na kusafirishwa katika magari maalumu kutegemea na uhitaji wa mazao hayo, na hupokelewa, kuchambuliwa na hatimaye kuhifadhiwa katika jokofu kubwa la baridi kuhakikisha kwamba ubora wa bidhaa unabakia kama ule wa shambani na baada ya hapo bidhaa hizo huuzwa kupitia duka hilo la kisasa na zingine hutumika katika mgahawa wao ambao pia unatengeneza aina mbali mbali za Juice nzito na nyepesi ambazo mara nyingi wataalam wa Afya wanashauri watu kutumia.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo ya Tomoni Farms Limited, Bwana Willybroad Alphonce amesema kuwa katika kufikia malengo na uendeshaji wameweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha cha Zaidi ya Bilioni moja.
Na kuongeza kuwa, wakiwa miongoni mwa Watanzania wazawa, wamewaomba watanzania kuwaunga mkono kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamemsaidia mkulima aliyoko kijijini ambaye bidhaa zake zinaharibika huku mijini zikihitajika kwa wingi, kwani licha ya wao kuendesha shughuli za kilimo pia wamekuwa wakinunua baadhi ya mazai kutoka kwa wakulima wengine ikiwa tu na lengo la kusaidia soko hasa la ndani.
“ Wateja watakao fika dukani kwetu watajipatia vitu mbalimbali. Ni wakati muafaka sasa kuchangamkia fursa hii ya bidhaa za mashambani ambazo zinatoka kwenye ardhi yetu ya nyumbani yenye rutuba za kutosha na uhifadhi wa hali ya usafi na usalama kwa mlaji.
Tunawakaribisha wote wanaotambua umuhimu wa kupata lishe bora kupitia matunda na mboga mboga huku tukiwasisitiza wale wote wenye watoto kuhakikisha wanawaleta pale Farm Fresh Bar waanze kuzoea toka mapema kuchangamana katika Bar zenye manufaa Kiafya” alimalizia
Tomoni Farms Limited inaendesha duka hilo la kisasa la mazao ya shambani, pia ina mgahawa na Bar maalum ambayo inahudumia bidhaa za matunda pekee ikiwemo juice za kila aina pamoja na masuala yote ya vyakula vya mboga mboga ambavyo ni vya asili.
DSC_8003 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani wakati wa utambulisho wa tukio hilo mapema leo Juni 23.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Bwana Willybroad Alphonce.
DSC_8013Muonekano wa nje unavyoonekana katika duka hilo la kisasa la bidhaa za shambani.
DSC_8045
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bw. Franklin Bagalla akifafanua jambo ndani ya duka hilo la kisasa la bidhaa za shambani
DSC_8047
Baadhi ya bidhaa zinavyoonekana ndani ya duka hilo.
DSC_8049 DSC_8057Baadhi ya mbogamboga za aina mbalimbali zikiwa zimehifadhiwa katika vifaa maalum
DSC_8059 DSC_8062Sehemu ya asili hasili inayotengenezwa na kampui hiyo
DSC_8071
Sehemu ya mchele na bidhaa zingine za nafaka zinazopatikana katika duka hilo.
DSC_8065sehemu ya matundaDSC_8074
Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya bidhaa za matunda yanayopatikana dukani hapo.
DSC_8079
DSC_8077 DSC_8089
Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya maboga bidhaa zinazopatikana dukani hapo.
DSC_8081
Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha mboga mboga za aina mbalimbali zinazopatikana dukani hapo.
DSC_8097Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha bidhaa maharage ya aina tofauti dukani hapo.
DSC_8099
DSC_8095
Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya bidhaa za asali dukani hapo.
DSC_8096Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya bidhaa za kalanga dukani hapo.
DSC_8086 DSC_8085 DSC_8093 DSC_8094 DSC_8117baadhi ya bidhaa zikiwa kwenye jokofu maalum zinapoifadhiwa.
DSC_8121Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akionyesha wanahabari (Hawapo pichani) bidhaa mahala zinapohifadhiwa katika jokofu maalum la matunda na mboga mboga.
DSC_8136Baadhi ya wanahabari na wadau wakijadiliana jambo nje ya kamouni hiyo ta Tomoni Farms Limited.
DSC_8148 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akiwa nje ya Bar maalum ya masuala ya matunda halisi pamoja na mbogamboga
DSC_8138 MatataG_4336Nje ya duka hilo la kisasa linavyoonekana lililopo katika jengo la Green House, eneo la jirani na Victoria, Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

1 comment:

Anonymous said...

SAFI SANA NAOMBA WATANZANIA TUMUUNGE MKONO HII SAFI KABISA,KWA KUNUNUA VITU FRESH NA KWA AFYA BORA ZETU NA FAMILIA ZETU