Saturday, June 4, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.tv:  Msongamano mkubwa wa wagonjwa katika taasisi ya ya mifupa MOI iliopo hospitali ya Muhimbili  kumesababisha kuzorota kwa huduma katika kitengo hicho ambapo msongamano huo unatokana na ajali za pikipiki. https://youtu.be/lM5yLRk0GAo  

SIMU.tv:  Wafanyakazi wa kampuni ya uzalishaji bia ya Serengeti SBL wameshiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu pamoja na kufanya usafi katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/yD2n7xvKT88  

SIMU.tv:  Wakazi wa kijiji cha Makani katika kitongoji cha Batini wilayani Bagamoyo wameulalamikia uongozi wa wilaya hiyo kwa kutowapa taarifa za kusitishwa kwa mkataba wa uekezaji wa kampuni ya Eco Energy iliokuwa imewachukulia ardhi ya zaidi ya ekari elfu 20. https://youtu.be/j8W5AN9uwUk
SIMU.tv:  Wananchi katika kata ya Nyakagwe katika wilaya ya Geita wameiomba serikali kuwatengenezea kipande cha barabara kinachoelekea kata ya Kakola ambacho kimeharibika kwa muda mrefu na kusababisha adha ya usafiri.https://youtu.be/3PBFvXP55pY

SIMU.tv:  Kijana Steven Geradi dereva wa bodaboda mkazi wa Ubungo aliyepigana na majambazi waliokua na silaha na kufanikiwa kuwathibiti amezawadiwa pikipiki aina ya boxer na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. https://youtu.be/fHzJ2kZd9QE

SIMU.tv:  Benki ya dunia imeridhishwa na mradi wa mabasi ya mwendo kasi nchini jijjni Dar es Salaam ambapo mwakilishi wake leo ametumia usafiri huo na kusifu huduma zake.https://youtu.be/vm6cyc-0Z2E

SIMU.tv:  Bodi ya shirika la umeme TANESCO imetakiwa kujikita katika kutafuta namna ya kuongeza mapato ya shirika hilo ili liweze kutatua changamoto ya madeni.https://youtu.be/GG6J80wOPBI   

SIMU.tv:  Benki ya Barclays imekua ya kwanza kufungua akaunti kwa kutumia mtandao ambapo akaunti ya mteja itafunguliwa kwa dakika ishirini tu.https://youtu.be/_Si7tF1fxVE
SIMU.tv:  Taifa stars inategemea kumenyana  na tumu ya taifa ya Misri hapo kesho ambapo inahitaji ushindi ili iweze kusonga mbele kwenye mashindano hayo.https://youtu.be/7c37PpkfNyI

SIMU.tv:  Mkoa wa Dar es Salaam umezindua rasmi mashindano ya UMISETA ili kutafuta timu zitakazo shiriki mashindano hayo ngazi ya taifa. https://youtu.be/FK04sXNrGw0

SIMU.tv:  Kikosi cha wanamaji cha jeshi la Nigeria pamoja na kikosi cha jeshi la Kenya kutoka kaunti ya Mombasa pamoja na vikosi mbalimbali hapa nchini vimethibitisha kushiriki katika mashindano ya ngumi ya mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam.https://youtu.be/sEkwzIi0oZ8
SIMU.tv:  Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Richard Martin maarufu kama Rich Mavoko jana amesaini mkataba wa kuwa chini ya lebo ya WCB ilioko chini ya mkurugenzi wake Diamond Platinumz. https://youtu.be/63va5jSwaZI

SIMU.tv:  Piere Emereke Aubameyang ametawazwa kuwa mchezaji bora wa ligi ya ujerumani maarufu kama Bundesliga. https://youtu.be/JiF-onMvNaM

SIMU.tv:  Operesheni ya kuwasaka wahalifu waliofanya uhalifu katika kijiji cha Kibatini Mkoani Tanga inaendelea huku wakazi wengi wakiwa wameyakimbia makazi yao;https://youtu.be/H6_MCFdt3M4
SIMU.tv:  Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Aggrey Mwanri ameitaka manispaa ya Tabora kumaliza mgogoro wa kiwanja cha TBC kilichovamiwa; https://youtu.be/120suWSJ6eE
SIMU.tv:  Baadhi ya wabunge wa CCM na anaibu waziri wa sera kazi vijana na walemavu Dr Abdallah Posi wamesema wabunge wanaotoka nje kumkwepa naibu spika ni uonevu wa kijinsia; https://youtu.be/tcSqMfch-tY
SIMU.tv:  Kituo cha uwekezaji nchini TIC kimekanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la The Economist la Uingereza  na Mwanahalisi la Tanzania kuwa serikali ya awamu ya tano haivutii wawekezaji; https://youtu.be/F_DFdoe-g4M
SIMU.tv:  Mke wa rais mama Janeth Magufuli amesema serikali inatambua umuhimu wa wazee na imejipanga kuwalinda na kuwatunza kikamilifu; https://youtu.be/V6r5eNqeNcs

SIMU.tv:  Mtoto Asha Mohamed mwenye umri wa miaka 9 wilayani Kinondoni anadaiwa kuwafanyiwa unyanyasaji kwa kumwagiwa maji ya moto usoni na mtu anayezaniwa kuwa ni mama yake wa kambo; https://youtu.be/T1P0L1AKKXI

SIMU.tv:  Bodi ya shirika la maendeleo la Ufaransa nchini imesema itaendelea kutoa misaada na mikopo yenye riba nafuu ili kusaidia maendeleo ya kiuchumi;https://youtu.be/qqd5iajgy4s

SIMU.tv:  Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na mfuko wa maendeleo wa Japan JAICA wamekubaliana kujenga upya soko la samaki la Malinzi; https://youtu.be/-fi_xzY5b9M

SIMU.tv:  Benki ya NMB na Ubalozi wa Uholanzi nchini limewakutanisha wanafunzi waliosoma Uholanzi na kuwapa maelezo jinsi ya kutunza fedha;https://youtu.be/wNvIKF8iaJk

SIMU.tv:  Benki ya Barclays nchini imeanzisha mfumo wa kufungua akaunti kwa njia ya mtandao kwa kutumia dakika 20 tu; https://youtu.be/Z332ODymNko

SIMU.tv:  Benki ya Posta nchini kuwasaidia waendesha bodaboda zaidi ya 100 wilayani Biharamulo mkoani Kagera; https://youtu.be/y2r-UfF6ND8

SIMU.tv:  Timu ya Taifa Taifa stars kesho jumamosi itashuka dimbani kuwavaana na timu ya Taifa ya Misri ili kuwania nafasi ya kucheza AFCON; https://youtu.be/NTNBQaPHSgg

SIMU.tv:  Mabondia watakaopanda ulingoni hapo kesho kuwania ubingwa wa UBO wametambia kutwangana na kuibuka na ushindi kwa kila mmoja; https://youtu.be/aWr-MwTp1p0

SIMU.tv:  Wasanii wa muziki nchini wametakiwa kusaidiana ili kuweza kuufikisha muziki wetu katika levo za kimataifa; https://youtu.be/c0fXhGkUP24

SIMU.tv:  Klabu ya Mbao Fc iliyopanda daraja msimu huu imesema haitotishika na ukubwa wa timu yoyote katika ligi hiyo na wao wamejipanga kuonyesha maajabu uwanjani;https://youtu.be/27_NAjwwSsY

SIMU.tv:  Kampuni ya Cocacola mkoani Katavi imetoa msaada wa vifaa vy michezo kwa timu zinazoshiriki mashindano ya Umiseta mkoani humo; https://youtu.be/jMVln7DiinM

No comments: