Wednesday, June 22, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa wito kwa bodi ya  mamlaka ya bandari nchini TPA kuboresha miundo mbinu ya utendaji katika bandari ya Dar es Salaam. https://youtu.be/YZ8SIdVJPjU

SIMU.TV: Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ametoa siku  kumi kwa maafisa wa wizara hiyo kutafuta suluhisho la mgogoro kati ya wakazi wa Magomeni kota na halmashauri ya manispaa ya Kinondoni. https://youtu.be/b8fW_a7SXFs

SIMU.TV: Waziri wa fedha Dr Philip Mpango amesema serikali itasimamia kikamilifu ukusanyaji wa kodi ili kuwezesha ufanisi katika zoezi hilo. https://youtu.be/NP2mPnr2_kE

SIMU.TV: Balozi wa Kuwait nchini ametoa msaada wa madawati 300 kwa serikali ya Tanzania ikiwa ni kuunga mkono jitihada za kumaliza tatizo la madawati.https://youtu.be/EJNhZRR8JS4

SIMU.TV: Wakazi waishio pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam wameliomba shirika la usafiri UDA kuwaongezea idadi ya mabasi ili kuwapunguzia adha ya usafiri inayowakumba.https://youtu.be/u-tLqFGOCJ0

SIMU.TV: Mfuko wa kichocheo wa taasisi ya kukuza kilimo kanda ya kusini mwa Tanzania umeingia mkataba na kampuni tano zitakazo wezesha kuwaendeleza wakulima wadogo.https://youtu.be/pFjo_Uyx-Uo

SIMU.TV: Mwenyekiti wa bodi ya uzalishaji wa sukari ya Kilombero amesema viwanda viwili vya kampuni hiyo vimeanza uzalishaji wa sukari itakayosaidia kuondoa uhaba wa sukari nchini. https://youtu.be/9YPhX77fHqY

SIMU.TV: Taasisi za fedha nchini zimetakiwa kuweka masharti rafiki kwa vijana kukopa ili kuwawezesha vijana kujiajiri. https://youtu.be/tBBwpq6Csv0

SIMU.TV: Nusu ya vijana nchini  wenye umri wa miaka 15 hadi 25 huishi bila kuwa na fedha za kutosha kukidhi mahitaji yao ya siku. https://youtu.be/neqtRQRV5nU

SIMU.TV: Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini maarufu kama Young D. amejitokeza hadharani na kutangaza kuacha kutumia madawa ya kulevya.https://youtu.be/nXVvx47AeEM

Shirikisho la soka nchini TFF limeandikia barua shirikisho la soka barani Afrika CAF kuliomba lisogeze mbele mchezo wa Yanga na TP Mazembe kutoka tarehe 28 na uchezwe tarehe 29. https://youtu.be/ZpU-kNnkA_I

SIMU.TV: Mabeki wawili wa Azam fc Shomari Kapombe na Pasco Wawa wamepelekwa Afrika kusini kupatiwa matibabu ili kujiandaa na mashindano yajayo.https://youtu.be/OWNed8T63VA

SIMU.TV: Marekani wamelala kwa kipigo kikali cha mabao manne kwa bila kutoka kwa Argentina kwenye nusu fainali za michuano ya Kopa Amerika.https://youtu.be/cvD0eB8t3lU

SIMU.TV: Bingwa wa dunia nchi ya Ujerumani wamejihakikishia kutinga hatua ya pili ya michuano ya EURO baada ya kuwalaza Ireland bao moja kwa bila hapo jana.https://youtu.be/YF7apl2R_XM

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli amesitisha rasmi ajira mpya serikalini sambamba na upandishwaji vyeo na madaraja kwa watumishi kwa muda ili kupisha zoezi la kuwaondoa watumishi hewa; https://youtu.be/hqjS6qge6Ro

SIMU.TV: Mahakama kuu kanda ya Iringa imetupilia mbali madai ya kuachiwa huru kwa mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mwandishi Daudi Mwangosi hivyo mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu; https://youtu.be/Ptnxz57RMrM

SIMU.TV: Takwimu za ajira kwa watoto nchini zinaonesha jumla ya watoto milioni 4 wanatumikishwa katika sekta mbalimbali sababu inayopelekea kukosa huduma za msingi ikiwamo elimu; https://youtu.be/orG2t-njI3U

SIMU.TV: Nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC zimekutana jijini Dar es salaam kujadili masuala mbalimbali juu ya usalama wa anga; https://youtu.be/MSlNw-1XMcE

SIMU.TV: Wadau wanaopinga kuendelea kwa ujangili dhidi ya Tembo katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda wamezishauri serikali za nchi hizo kuungana kwa pamoja kumaliza tatizo hilo; https://youtu.be/SCsIMqaFgOA

SIMU.TV: Diwani wa kata ya Nyamkumbi wilayani Geita amekumbwa na msukosuko baada ya kuitisha mkutano na kutaka kuwachagulia wananchi  mabalozi kwa mwamvuli wa chama chake; https://youtu.be/-4RRIKFatlY

SIMU.TV: Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji ameliagiza shirika la viwango na tume ya ushindani nchini kuhakikisha bidhaa feki hazizalishwi wala kuingizwa nchini;https://youtu.be/WtGipXjYLyg

SIMU.TV: Zaidi ya wakulima elfu 70 kusini mwa bara la Afrika wanatarajia kunufaika na mradi wa uzalishaji wa mazao ya chakula barani Afrika; https://youtu.be/sJVgxxDgYKs

SIMU.TV: Makampuni matano yanayoshughulika na kilimo hapa nchini yametiliana saini hii leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kukuza bidhaa za kilimo nchini Tanzania;https://youtu.be/e3Nihtp_qZ4

SIMU.TV: Mchezo wa hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Yanga na TP Mazembe unatarajia kufanyika tarehe 28 mwezi huu jijini Dar es salaam;https://youtu.be/-5uZHsVlCCI

SIMU.TV: Katika kukuza sekta ya michezo mkoani Mara, chama cha soka mkoani humo kinajiandaa kufanyia marekebisho uwanja wa Karume mkoani humo kujiweka sawa kwa mashindano mbalimbali; https://youtu.be/bymWwdAM_oo

SIMU.TV: Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na kukosa menejimenti ya uhakika msanii Young Dee ametangaza kurudi katika lebo yake ya zamani ya MDB chini ya meneja Max Rioba; https://youtu.be/fLmPGmGRsGU

SIMU.TV: Mshambuliaji nyota wa timu ya taifa ya Sweden na klabu ya PSG Zlatan Ibrahimovich ametangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya EURO inayoendelea nchini Ufaransa; https://youtu.be/eyni-gdHOGw

No comments: