Tuesday, June 21, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Wananchi wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wamemuomba waziri mwenye dhamana ya kilimo nchini kuingilia kati mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na mwekezaji; https://youtu.be/BLfNIxzOYvQ

SIMU.TV: Kampuni ya BAM inayojenga uwanja wa ndege jijini Dar es salaam imetoa msaada wa madawati katika jitihada za kuunga mkono agizo la rais la kumaliza tatizo la madawati nchini; https://youtu.be/CXzTdZvkOOQ

SIMU.TV: Jumla ya walengwa 180 wa mradi TASAF wilayani Maswa mkoani Simiyu wamejiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya kwa jamii; https://youtu.be/sp5n1TGPiRo

SIMU.TV: Familia moja imeleta kizaazaa nyumbani kwa mchungaji David eneo la Magomeni jijini Dar es salaam baada ya kukaa na ndugu yao kwa muda wa miezi mitano bila taarifa kwa familia hiyo; https://youtu.be/AJn-7t2gHsM

SIMU.TV: Halmashauri ya Kahama mkoani Shinyanga imekamilisha zoezi la utengenezaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari baada ya kampuni ya madini ACACIA kukabidhi madawati 1380; https://youtu.be/i8SLdy7O2KQ

SIMU.TV: Benki ya CRDB imewazawadia wateja wake wanaotumia kadi za Tembocard katika kufanya manunuzi ya bidhaa kwa kutumia kadi hizo; https://youtu.be/0J7ApQQtT40

SIMU.TV: Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imezindua mfumo mpya wa huduma  ya M-Pepa kwa wateja wake baada ya kuwawezesha kusoma magazeti kupitia simu za mkononi; https://youtu.be/--zX7pqQvMo

SIMU.TV: Taasisi za kifedha nchini zimeendelea kuunga mkono juhudi za serikali nchini katika kuwezesha wananchi wa ngazi zote wanamiliki makazi kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu; https://youtu.be/UC0-SlMi_Ck

SIMU.TV: Timu ya soka ya vijana Serengeti boys imeendelea kujifua mazoezi kujiandaa na mchezo wake dhihi ya timu kutoka Shelisheli siku ya Jumapili;https://youtu.be/8JN2C73wvjE

SIMU.TV: Rais wa klabu ya soka ya Lipuli mkoani Iringa Jesca Msambatavangu amewataka viongozi wanaovutana kukaa meza moja kumaliza tofauti zao ili kuijenga timu yao;https://youtu.be/8y7cPc_g5eI

SIMU.TV: Serikali imeombwa kuwadhibiti wanamichezo wenye tabia ya kuongeza nguvu michezoni ili kuwezesha ushindani na kupata washindi wa haki;https://youtu.be/sA95AXx3Yrs

SIMU.TV: Kamati ya Olimpiki duniani inaendelea kujadili suala la kuifungia nchi ya urusi kushiriki mashindano hayo baada ya wanariadha yake kukutwa na hatia za kutumia dawa michezoni; https://youtu.be/vr0wi4zRmeE

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema serikali itaendelea kufanya ukarabati wa mara kwa mara na uundaji wa vivuko vipya kwa maeneo yote yanayotumia usafiri huo. https://youtu.be/SdElItmTh4I

SIMU.TV: Wakazi wa kata ya Nanyanga katika wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara wamekusanya  kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 17 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.https://youtu.be/AD6I5iiFsZ4

SIMU.TV: Hospitali ya taifa ya Muhimbili imeingia ubia na mzabuni ambaye atatoa huduma ya chakula kwa wagonjwa watakaokuwa wamelazwa hospitalini hapo.https://youtu.be/x0XIAZn6AS8

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli amemteua Dr Jim James Yonazi kuwa mhariri mtendaji wa kampuni ya  magazeti ya serikali TSN. https://youtu.be/TYwBUWn_vZk

SIMU.TV: Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Mbijima amezishauri halmashauri nchini kuzingatia agizo la kutenga fedha kwa ajili ya mikopo kwa vijana na wanawake. https://youtu.be/HXskbVt6H9w

SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake wajasiriamali nchini kujiunga na majukwaa ya wajasiriamali nchini  ili kupata elimu ya kujiinua kiuchumi.https://youtu.be/Yh9kG_HdyCw

SIMU.TV: Wakulima wa mazao jamii ya mikunde katoka kanda ya kaskazini wameshauriwa kulima kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo ili kuweza kujipatia mavuno mengi.https://youtu.be/D-13625EDmk

SIMU.TV: Mamlaka ya vyakula na dawa nchini TFDA katika nyanda za juu kusini imesema bidhaa nyingi katika maeneo hayo hazina usajili. https://youtu.be/IYgzol9IRX8

SIMU.TV: Benki ya ACB imeongeza idadi ya mikopo ya kuboresha maisha iliyotolewa  kwenye kipindi cha kuanzia mwaka 2014 hadi 2015. https://youtu.be/CThsqwW_z0w

SIMU.TV: Benki ya Diamond Trust imeandaa mpango wa kutoa mikopo ya bei nafuu kwa wateja wake. https://youtu.be/UGxN60tKUeA

SIMU.TV: Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imezindua huduma ya kidigiti ya kusoma magazeti kwa wateja wake ambayo itamwezesha kusoma magazeti kwenye mtandao huo. https://youtu.be/qPfyNx_9mp0

SIMU.TV: Wawikilishi pekee wa michezo ya Shirikisho barani Afrika timu ya Yanga imeamua kurudi nchini Uturuki kwa maandalizi zaidi ya mashindano hayo.https://youtu.be/5e5vSdN9yTA

SIMU.TV: Baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Arusha wamekabidhi vifaa vya michezo kwa timu za Shambalai Fc na Mbuguni Fc. https://youtu.be/Xk7MfGkQ7qc

SIMU.TV: Wales wameongoza kundi B baada ya kuilaza timu ya Urusi mabao matatu kwa bila katika fainali za mataifa ulaya maarufu kama EURO. https://youtu.be/3g21V0256HM

SIMU.TV: Nusu faina za kopa Amerika zinaanza kutimu vumbi kesho wakati Marekani itawaalika Argetina. https://youtu.be/_1A2vq8EkPo

No comments: