Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipokea Mwenge wa Uhuru toka kwa Mkuu wilaya ya Mufindi Jolwika Kasunga katika kijiji cha Ikungwe kata ya Wasa tarafa ya Kiponzelo.
Mwenge huo ambao ulikimbizwa zaidi ya Km 11.5 katika vijiji 7, kata 4 na tarafa 2. katika mbio hizo jumlay amiradi 5 ya wananchi ilizinduliwa, miradi 5 ya vijana ilizinduliwa pia klabu 2 za Rushwa na mapambano ya madwa ya kulevya harikadharika vilizinduliwa.
Kiasi cha shilingi milion 15 zilitolewa kwa vikundi 5 vya vijana kama ilivyo kauli mbiu ya Mbio za Mwenge mwaka 2016 VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA WASHIRIKISHWE NA KUWEZESHWA.
Taarifa yake Mkuu wa wilaya Iringa pamoja na risala ya Utii kwa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kasesela alisema Halmashauri ya Iringa vijijini imetenga hekali 198 kwa ajili ya shughuli za maendeleo za vijana, katika vijiji 10 kwa ajili ya ujasiliamali.
Halmashauri imefanikisha vijana 1321 kupata ajira kwenye miradi ya kijamii, 1230 walipata ajira zilizo tokana na wazabuni hasa hasa wa ujenzi wa barabara na miundo mbinu ya mwaji. sambasamba na hilo pia vijana 28, 783 wamewezeshwa kujiajiri ambapo wengi ni katika kilimo.
Mwenge ulifanikiwa kuonwa na kuguswa na watu karibu 1880 kwa kadirio la haraka. Mwenge wa uhuru ulilala Ifunda ambapo mkesha wa Mwenge uliudhuriwa na watu karibu 300 mpaka asubuhi.
Kivutio kikubwa kilikuwa watoto wa halaiki walivyoonyesha ukakamavu . Mwenge ulikabdhiwa wilaya ya kilolo kuendelea na mbio hizo. Unatarajiwa kurudi Iringa Manispaa tarehe 22/06/2016 na kupokelewa tena na Mh Richard Kasesela eneo la Tagamenda saa 2 asubuhi.
Mh Jolwika Kasunga DC wa Mufindi akimkabidhi DC wa Iringa Mh Richard Kasesela Mwenge wa uhuru
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bwana George Jackson Mbijima na Mkuu wa wilaya Iringa wakipookea heshima kutoka kwa chipukizi
Watoto wa haraiki walivyoonyesha ukakamavu
Mwenge ukianza mbio rasmi Iringa
Mzee chavala ambaye ni mstaafu aliwahi kufanya kazi na Bwana George Mbijima mkimbiza mwenge Taifa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiwapagaisha wananchi wa Ifunda kwa kuchana mistari na kuzindua wimbo alioshirki kuimba wa Mwenge Tanzania alioimba na msanii D Money. Vumbi lilitimka kama linavyo onekana
DC Kasesela akipagawisha wananchi wa Ifunda
Ngoma inogile
Mchekeshaji Ali yanga alishiriki katika kuchangisha wananchi hela za madawati ambapo hadi tunaenda mitamboni zilifika 232,000/- na michango inaendelea.
Furaha ya mwenge
Furaha ya mwenge
msanii wa kizazi kipya D Money akiwapagaisha wananchi waliojitokeza kwenye mkesha wa Mwenge
No comments:
Post a Comment