Thursday, June 2, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu Sera Kazi na vijana Mh Jenista Mhagama ameelezea hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya kutokea kwa mauaji ya Tanga;https://youtu.be/t1RJFGN-i5c

SIMU.TV: Wakazi wa kijiji cha Kibatini mkoani Tanga wameiomba serikali kuwaamisha sehemu hiyo kufuatia kutokea kwa mauaji ya watu wanane hapo jana;https://youtu.be/XM18mEXhpAU

SIMU.TV: Waziri wa Fedha na Mipango Dr Philip Mpango amesema dhamira ya serikali katika kuifikia nchi ya uchumi wa kati iko pale pale; https://youtu.be/USxb7vmvOFo

SIMU.TV: Wilaya ya Babati mjini mkoani Manyara imebaini ubadhirifu wa fedha zaidi ya shilingi bilioni 1 katika mradi wa ujenzi wa barabara; https://youtu.be/0yQl8vEq0S8

SIMU.TV: Naibu waziri wa TAMISEMI Mh Suleiman Jaffo ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa wote wanaosuasua katika kutimiza agizo la madawati wakamilishe ndani ya wiki chache zilizosalia; https://youtu.be/tuhR75Q59L4

SIMU.TV: Kampuni ya ving’amuzi ya Startimes na Shirika la utangazaji nchini TBC imepata tuzo ya ubora wa urushaji matangazo nchini; https://youtu.be/sTEC154Da_Q

SIMU.TV: Waziri wa viwanda na biashara Zanzibar Amina Salum amewataka wafanyabiashara visiwani kutopandisha bei bidhaa kipindi cha mfungo wa ramadhani;https://youtu.be/Tt-vO-YfVzY

SIMU.TV: Mchakato wa kuzipata kampuni 100 za Tanzania zenye mtaji kuanzia bilioni 1 umeanza rasmi nchini ; https://youtu.be/F-yOYkCkGaE

SIMU.TV: DAWASCO wameendelea na operesheni ya kukata maji kwa wateja waliojiunganishia maji kinyume cha sheria na kuwachukulia hatua;https://youtu.be/g0cA551Gvmg

SIMU.TV: Baadhi ya wafanyabishara wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wamesusia kikao cha baraza la madiwani kupinga bei kubwa ya pango kwa vibanda vya biashara wilayani humo;https://youtu.be/JVfjmNKd8j8

SIMU.TV: Sakata la uchaguzi katika klabu ya Yanga limechukua sura mpya baada ya uongozi wa klabu hiyo kuibuka na kuitangaza kamati yake ya uchaguzi kinyume na ile ya TFF iliyopewa dhamana ya kuratibu uchaguzi huo ; https://youtu.be/aMHbRN8BCPE

SIMU.TV: Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imesema tatizo la kubadilishwa kwa ratiba ya ligi kuu mara kwa mara halitojirudia tena msimu ujao; https://youtu.be/jG8JGXCXv3s

SIMU.TV: Shirikisho la ngumi za kulipwa nchini PST limesema wanasubiri kupokea barua yao ya kufungiwa ili waende kukatan rufaa; https://youtu.be/0929q70gPjo

SIMU.TV: Mshambuliaji wa zamani wa kikosi cha Uingereza Allan Shearer amekosoa uteuzi wa kikosi cha taifa cha Uingereza kinachokwenda kushiriki michuano ya EURO nchini Ufaransa; https://youtu.be/V76lg0t5_4A

SIMU.TV: Mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Eslalei kwenye kata ya Eslalei wilayani Monduli umeendelea kuchukua sura mpya baada ya wananchi kuitaka serikali kuwapa hati miliki ya shamba la SIMU.TV: Manyara Ranch na kusema wanashangaa wanasiasa kumhusia Lowassa kuhusika na umiliki wa shamba hilo. https://youtu.be/9OwaW_Cd7UA 

SIMU.TV: Wahamiaji haramu 71  raia wa Ethiopia wamekamatwa jijini Dar es Salaam eneo la Kigamboni baada ya kupakiwa kwenye lori la migizo ili waweze kusafishwa kuelekea Afrika kusini. https://youtu.be/VNtwrJ2-AIU

SIMU.TV: Nchi mbali mbali zimekutana nchini ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utawala bora  na sheria ambapo Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo. https://youtu.be/oINPjokGQnY

SIMU.TV: Wakazi wa Ilala Kota jijini Dar es Salaam wapo hatarini kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na mfereji wa maji taka kutiririsha maji machafu kwenye makazi ya wananchi hayo. https://youtu.be/l0W7G5ozibI

SIMU.TV: Wananchi wa kata ya Iwambala kata ya Uyole katika halmashauri ya jiji la Mbeya wamemnyang’anya mwekezaji shamba walilompa kwa ajili ya ujenzi wa shule tangu 2003 lakini mpaka sasa ameshindwa kutekeleza azma yake hiyo. https://youtu.be/WtSoYF4Xxlg

SIMU.TV: Wazee kutoka jamii ya wafugaji na wakulima katika wilaya ya Kiteto wameamua kula kiapo mbele ya viongozi wa serikali ili kumaliza mauaji na migogoro ya ardhi inayowaathiri katika wilaya hiyo. https://youtu.be/TSb702I1lSg

SIMU.TV: Jumla ya makampuni 250 ya biashara za kati yanatarajiwa kuteuliwa kwenye mchakato wa kuyapata makampuni 100 bora katika biashara za kati nchini.https://youtu.be/J0xVrnCpgd0

SIMU.TV: Licha ya tafiti nyingi kufanyika namna ya kuboresha kilimo bado magonjwa ya mazao yanaonekana kushambuli a kilimo ambapo kwa sasa bioteknolojia inaonekana kuwa njia itakayo leta mafanikio kuthibiti changamoto hio.https://youtu.be/ytfpAbtWH6M

SIMU.TV: Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa ufafanuzi wake kuelekea uchaguzi mkuu wa viongozi wa ngazi za juu za klabu hiyo. https://youtu.be/WEMZaC55qh0

SIMU.TV: Timu ya Mbeya city inatarajia kufanya ziara ya kimichezo katika nchi ya Malawi mabapo watacheza michezo ya kirafiki ikiwa ni njia ya kujiimarisha kwa msimu ujao wa ligi kuu. https://youtu.be/fC1ssF8ZvDg

SIMU.TV: Ukata wa fedha umekua changamoto kubwa inayoikabili michezo ya UMISETA katika mkoa wa Katavi inayohusisha halmashauri nne za mkoa huo.https://youtu.be/ui1gy09VyAI

SIMU.TV: Wasanii wa ngoma za asili mkoani Ruvuma wameiomba serikali kurudisha somo la utamaduni mashuleni ili kuweza kuwarithisha watoto utamaduni wa chimbuko lao.https://youtu.be/P__Jrz8kWhk

SIMU.TV: Wasanii mbalimbali wanatarajia kunufaika na kazi zao kutokana na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ikishirikiana na Global Publishers kuzindua huduma maalu ya kuwezesha wateja wake kupata taarifa muhimu kuhusu wasanii hao.https://youtu.be/YgzBIgmEnak

SIMU.TV: Michuano ya soka maarufu kama Ndondo cup inayodhaminiwa na tabibu Mwaka inatarajiwa kuingi katika hatua ya pili ambapo timu shiriki zimekabidhiwa vifaa vya michezo. https://youtu.be/CX5opYCVTSw

SIMU.TV: Timu ya taifa ya Ireland jana ilipata matokeo mabaya kwenye mchezo wa maandalizi ya Euro pale ilipo fungwa na timu ya taifa ya Belarus.https://youtu.be/BK9lZY8sNSQ

No comments: