Wednesday, June 15, 2016

Migogoro ni chanzo cha kudidimia kwa Uchumi wa Afrika


Benjamin Sawe -Maelezo
Dar es Salaam

Amani ni msingi wa maendeleo na hivyo ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.Bila amani,nchi haiwezi kufanya shughuli za maendeleo hata pale ambapo maendeleo yameshapatikana,huweza kuvurugwa endapo amani itatoweke katika nchi.

Nchi ambazo kwa miaka ya hivi karibuni zimejitaidi kupiga hatua za maendeleo na zinaendelea kufanya jitiada kuhakikisha kuwa zinapiga hatua kubwa zaidi ya maendeleo kwa faida ya wananchi wote,jitiada hizo pia,kwa baadhi ya nchi zimeathiriwa na migogoro.

Matokeo ya migogoro hiyo ni mamilioni ya waafrika wasio na hatia kupoteza maisha yao na mamilioni zaidi kujeruhiwa.Pia mamilioni ya wanawake na watoto kupatwa shida kubwa na baadhi ya watu kukimbia nchi zao na kukimbilia nchi za jirani katika kuokoa maisha yao hivyo kujikuta wakiishi maisha ya dhiki nje ya nchi yao.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2009,Afrika ilikuwa na wakimbizi milioni 3 ambayo ni asilimia 20 ya wakimbizi wapatao milioni 10.5 duniani.Aidha,Afrika inakisiwa kuwa ina watu milioni kumi na mojana laki sita ambao wamelezimika kuhama makazi yao kwa ajili ya vita

Migogoro migogoro huwa kikwazo kikubwa cha shughuli za maendeleo siyo tu kwa watu binafsi bali pia kwa taifa.Fedha ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye huduma muhimu ya jamii kama afya,elimu,maji ni fedha ambazo huelekezwa katika manunuzi ya silaa.

Inakadiriwa kuwa hasara ya kiuchumi inakadiriwa kuwa wastani wa dola bilioni kumi na nane kwa kila mwaka sababu ya migogoro.

Hali hii ya migogoro katika bara la Afrika imelifanya bara hili kujulikana kama bara la mapigano jambo ambalo ni dhahiri linasikitisha hivyo hatuna budi kuondokana na hali hiyo ya migogoro na kuwa bara huru lisilo na migogoro.

Ni kweli kuwa katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko,kutokana na juhudi zilizofanyika,Afrika imefanikiwa kupunguza idadi ya migogoro kuliko ilivyokuwa katika miaka ya 1980 wakati ambapo nchi nyingi zilikuwa na migogoro

Mfano nhci kama Liberia,Sierra Leone,Msumbiji,Angolo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),Burundi na Comoro nazo zimeendelea kuimarisha amani,Hali hii inatupa faraja lakini bado Bara la Afrika linamigogoro kama vile ya Somalia na Darfur kuko Sudani.

Mgogoro wa Somalia ni mgogoro wa muda mrefu sasa ambao ni changamoto kubwa kwa bara la Afrika na jamii ya Kimataifa kwa ujumla na hivyo unahitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi.

Hali ya usalama nchini Somalia ambayo kwa takribani miaka ishirini sasa imekuwa katika mazingira ya kusikitisha kwa takribani miaka ishirini sasa imekuwa katika mazingira ya kusikitisha ambapo kwa ujumla usalama wa wananchi wan chi hiyo umo katika hali ya hatihati.

Kwa upande Tanzania tunafahari kubwa ya kuwa mstari wa mbele katika kujenga mazingira yetu wenyewe ya kuwa na amani,utulivu na mshikamano na pia katika kusaidia ndugu na majirani zetu na sehemu nyingine za Bara la Afrika katika kufanukisha lengo la kuleta amani popote pale inapokosekana.

Sote tunatambua kuwa Serikali ya Tanzania katika kutetea amani katika bara la Afrika imepeleka vijana wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) katika miaka ya nyuma walikwenda nchini Liberia kwa lengo hilo.Na hivi karibuni wanajeshi wetu wamekwenda Darfur kuungana na wanajeshi wengine wa Kiafrika na nchi nyingine chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Vilevile,viongozi wetu wa Afrika wameshiriki na wanaendelea kushiriki kutoa michango yao muhimu katika juhudi juhudi za kuleta amani.

Mfano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa jakaya Kikwete ametoa mchango muhimu katika kumaliza mgogoro wa ndugu zetu wa Kenya uliotokana na uchaguzi uliofanyika nchini humo mwaka 2007.

Pia Rais mstaafu wa awamu ya tatu,Mheshimiwa Benjamin Mkapa ametoa na anaendela kutoa mchango wake katika juhudi za kurudisha amani na utulivu huko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na hasa mgogoro w mashariki ya Kongo.

Mkapa anazitaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhakikisha nazo zinaendelea kusaidia nchi ya Burundi ili amani ipatikane.

Anasema wenye jukumu la kuleta amani kwa nchi yao ni Warundi wenyewe na kuwataka kukaa meza moja ili kujadiliana pamoja na kuondoa tofauti zao na amani ni kitu muhimu kwa mustakabali wa nchi ya Burundi, hivyo ni vyema wakatumia mkutano huo vizuri kufikia muafaka.

Mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa, Balozi Roeland Van der Geer akizungumza kwa niaba ya jumuiya hiyo anasema nchi ya Burundi inatakiwa kuhakikisha amani inapatikana ili kuhakikisha kila raia wa nchi hiyo anapata maendeleo.

Aidha mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika katika nchi za Maziwa Makuu, Balozi James Benomaar alisema jumuiya hiyo ina imani kubwa na Rais Mkapa katika kusuluhisha mgogoro huo na kutoa rai kwa Warundi kuhakikisha wanamaliza mgogoro wa nchi yao ili kupunguza wimbi la wakimbizi wanaokimbilia nchi mbalimbali kwa usalama wa maisha yao.

Inasikitisha kuona bara letu la Afrika kutangazwa kama ni bara la mapigano hivyo ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha kuwa amani yetu inaendela kudumu na kuhakikisha amani yetu inaendelea kulindwa na inapatikana katika maeneo mengine barani Afrika.

No comments: