Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bw.Harrison Chinyuka akizungumza na Viongozi wa vikundi vya mradi huo (hawapo pichani) walipotembelea Kata ya Makanya Wilaya ya Same kukagua utekelezaji wa mradi huo Juni 14, 2016.
Afisa Mtendaji Kata ya Makanya Bw.Josephat Kitunga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Kata yake alipotembelewa na Wataalamu wa masuala ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ili kukagua miradi inayotekelezwa, tarehe 14 Juni, 2016.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Herman Kapufi (katikati) akizungumza na baadhi ya Wadau wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame walipotembelea Wilaya hiyo kuangalia utekelezaji wa mradi katika kata ya Makanya, Vunte na Hedaru Mkoani Kilimanjaro.
Mchumi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Magreth Sembuyagi akifafanua jambo walipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Same Bi. Monica Kwilulihya (hayupo pichani) ili kuendelea na shughuli za kukagua miradi inayotekelezwa na Ofisi hiyo.
Mnufaika wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bi.Neema akifurahia mafanikio ya kununua ng’ombe mara baada ya kuuza kuku aliozalisha kupitia mradi huo katika Kata ya Makanya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, tarehe 14 Juni, 2016.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Ujamaa Bi. Khadija Mrutu akihudumia mifugo aliyozalisha kupitia Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kutembelewa na Wadau wa mradi huo kwa kufanya tathimini za utekelezaji wake.
No comments:
Post a Comment