Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimpa pole
Hussein Mkola ambaye ni mtoto wa marehemu Mkola Hussein ambaye alichinjwa na watu
wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya
Mzizima, mkoani Tanga. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni
linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia nane
zilizofiwa katika kitongoji hicho.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo wakati alipokuwa anawasili msibani katika
Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga, ambapo watu wanane walichinjwa na
watu wanaohofiwa kuwa majambazi. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya
Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika
familia hizo zilizofiwa katika kitongoji hicho. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali
Davis Mwamunyange.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwapa pole
wanafamilia ya marehemu Mkola Hussein ambaye alichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa
majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani
Tanga. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni
njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia nane zilizofiwa katika
kitongoji hicho. Nyuma ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis
Mwamunyange.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo akiwaonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis
Mwamunyange (wapili kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu (watatu
kushoto), nyumba ya kwanza katika Kitongoji cha Kibatini walioivamia watu wanaohofiwa
kuwa majambazi na kufanya mauaji. Naibu Waziri na Viongozi hao walienda kutoa pole katika
familia zilizofiwa katika Kitongoji hicho kilichopo katika Kata ya Mzizima, mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa salamu za pole
kwa ndugu wa marehemu Mkola Hussein pamoja na wananchi wa Kitongoji cha Kibatini
kulipotokea mauaji kwa watu wanane ambao walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa
majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji hicho kilichopo Kata ya Mzizima, mkoani
Tanga. Katika hotuba yake Masauni alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo na itahakikisha
inawakamata wauaji wote waliofanya ukatili huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakijadiliana
jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange kabla ya kwenda kutoa
pole kwa familia ya wafiwa katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga
ambapo watu wanane walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi. Picha zote na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment