Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akipokea salamu wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa maofisa 27 wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akikagua gwaride la maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakati wa kufunga mafunzo yao katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) wakila kiapo cha utii wakati wa kumaliza mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akiwa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa TANAPA,Witness Shoo wakifuatilia maonesho ya kijeshi kutoka kwa maofisa wa ngazi za juu wa shirika hilo waliomaliza mafunzo katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe na wageni wengine waalikwa wakiangalia umahiri wa maofisa wa Tanapa namna walivyopata mafunzo ya kijeshi ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kutoka ule wa kiraia kwenda mfumo wa jeshi Usu.
Maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) waliomaliza mafunzo ya kijeshi wakiwa wamebeba silaha kuonesha utayari katika kupambana na ujangili katika Hifadhi za Taifa .
Maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakionesha umahiri katika kulenga Shabaha wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa maofisa hao yaliyofanyika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Waziri wa maliasili na Utalii ,Prof Jumanne Maghembe akitizama matundu ya risasi wakati wa zoezi la ulengaji shabaha kwa maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,mafunzo yaliyofanyika kambi la Mlele mkoani Katavi.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Pascal Shelutete akitoa muongozo wa namna wahitimu wa mafunzo hayo watakavyo pokea vyeti mara baada ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa maofisa wa ngazi za juu wa Shirika hilo ,mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Mkuu wa wilaya ya Mlele ,Kanali Mstaafu ,Issa Njiku akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) .
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa maofisa wa ngazi ya juu katika Shirika hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akitoa hotuba yake wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa maofisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Hifadhji za Taifa (TANAPA) mafunzo yaliyofanyika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibooki akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri Maghembe kufunga mafunzo kwa maofisa wa ngazi za juu wa shirika hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof,Jumanne Maghemnbe akifurahia jambo na maofisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Maofisa Uhifadhi wa ngazi ya juu katika Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof,Jumanne Maghembe mara baada ya kufunga mafunzo kwa maofisa hao.
Maofisa Uhifadhi wa ngazi ya juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele iliyoko mkoani Katavi.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.
1 comment:
The mdudu, safi sana sasa uzalendo mbele kwa mbele malizeni majangili wote maana hakuna jinsi
Post a Comment