Thursday, June 2, 2016

Mama Magufuli amshukuru Mtumishi wa Mungu TB JOSHUA kwa kuunga mkono Jitihada zake za kusaidia wazee

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Chama na Wazee wakati akiwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi pamoja na Vifaa vya Malazi.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Chama na Wazee wakati akiwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi pamoja na Vifaa vya Malazi.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa  Mtwara Mh. Halima Dendegu baada ya kuangalia nyumba zinazojengwa na kufanyiwa marekebisho kwa ajili ya makazi ya wazee wa kituo cha Nkaseka Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi, Madawa pamoja na Vifaa vya Malazi.
 Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara
 Baadhi ya Wazee walimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
 Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akimueleza jambo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla ya utoaji misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Nkaseka Mkoani Mtwara.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akicheza ngoma na moja ya kikundi cha kinamama Mkoani Mtwara wakati wa hafla ya utoaji wa misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Nkaseka Mkoani Mtwara.
 Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Bw. Rashidi Kambona akiwashukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa kwa kutambua umuhimu wa kusaidia wazee katika kituo hicho na kutoa misaada itakayowapunguzia machungu ya mahitaji maalum wazee hao.
 Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Bw. Rashidi Kambona akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akiongea na wazee na baadhi ya watu waliojitokeza katika hafla ya utoaji Misaada katika kituo cha kulea Wazee cha Nkaseka Wilayani Masasi Mkoani Mtwara na kumshukuru Mama Janeth Magufuli kwa misaada hiyo na kumuahidi kusimamia ugawaji wa vitu hivyo ili kuepuka kuchukuliwa na watu wasiowaaminifu.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akicheza na viongozi Wanawake wa Mkoa wa Mtwara.
 Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akiongea na Wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
 Muwakilishi wa Mtumishi wa Mungu TB Joshua Nchini Tanzania Mhandisi Consolata Ngimbwa akitoa salamu kutoka kwa TB Joshua aliyetoa msaada kwa ajili ya wazee wa kituo cha Nkaseka kilichopo Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wazee katika kituo cha Nkaseka Mkoani Mtwara na kumshukuru Mtumishi wa Mungu TB Joshua kuunga mkono juhudi zake za kuwasaidia wazee na watu wasiojiweza kwa kuchangia baadhi ya vitu vilivyotolewa kama msaada kwenye kituo hicho.
 Kiongozi wa Wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka Bw. Boniface Mbedo akiwashukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa kwa misaada waliyotoa na uamuzi wa kukitembelea kituo hicho.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Kiongozi wa Wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka Bw. Boniface Mbedo misaada leo Mkoani Mtwara.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo na moja ya Mzee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka baada ya kumpa zawadi ya Ungo, Chungu na Mwiko. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa, wakati wa hafla ya utoaji misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Nkaseka Mkoani Mtwara.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka kilichopo Mkoani Mtwara.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (Kushoto) na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa wakimsalimia Moja ya Mzee katika Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka kilichopo Mkoani Mtwara.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo na baadhi ya watoto waliojitokeza katika hafla ya utoaji msaada katika Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka kilichopo Mkoani Mtwara. PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

1 comment:

Anonymous said...

Good morning Tanzania.. Emmanuel..