Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), Steven Ruvuga (kulia) akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Maji, kuhusu matatizo mbalimbali wanayopata wakulima na wafugaji nchini, wakati wa mdahalo wa kujadili changamoto zinazowakabili kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa, Dodoma
Mfugaji ambaye ni Mjumbe wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), Trugeti Kashu kutoka Mbarali, mkoani Mbeya, akielezea mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Maji, Bungeni Dodoma jana, kuhusu migogoro ya wafugaji na askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Ruaha ambapo mifugo yao hutekwa na kuwalipisha fedha nyingi kuigomboa. Mviwata walikutana na wajumbe wa kamati hiyo, bungeni Dodoma
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), Veronica Sophu
(kulia) akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, kuhusu matatizo mbalimbali wanayopata wakulima na wafugaji nchini, wakati wa mdahalo wa kujadili changamoto hizo kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa, Dodoma
Wakulima wakinyoosha mikono ili waeleze changamoto zinazowakabili mbele ya wabunge
Wajumbe wa Mviwata akisikiliza kwa makini wakati Mwenyekiti wa Kamati, Mary Nagu akifungua mjadala huo.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Maji wakisikiliza kwa makini wakati wakulima wakielezea changamoto zao
Mkurugenzi Mtendaji wa Mviwata akifafanua jambo katika mdahalo huo
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kilimo, Dk. Mary Nagu akichangia hoja katika mdahalo huo hasa kuhusu matumizi bora ya ardhi tuliyonayo ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji nchini.
Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Bobali akiwapongeza wajumbe wa Mviwata kwa kazi nzuri wanayofanya kuhakikisha wakulima wanendelezwa.
Mbunge wa Mkuranga, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, akichangia hoja kwa kuwapongeza Mviwata.
Mbunge wa Mbozi,Pascal Haongaakichangia hoja wakati wa mjadala huo
Mbunge wa Jimbo la Mufindi, Mahamoud Mgimwa akielezea jinsi alivyoshiriki kutatua migogoro ya wakulima, wafugaji na askari wa wanyamapori alivyokuwa NMaibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
Mbunge wa Jimbo la Makambako, Deo Sanga akichangia katika mjadala huo
Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philip Mulugo akchangia hoja na kutaka wakulima hao wakutanishwe haraka na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba ili ashiriki kutatua changamoto hizo
Mmmoja wa wakulima akielezea matatizo mbalimbali yanayowakabili
Nsanzugwako akijibu baadhi ya hoja za wakulima
Ruvuga akifafanua jambo huku akisikilizwa kwa makini na Nsanzugwako
Mkulima Antonia Edward kutoka Kilosa , akiitaka serikali kuharakisha mpango wa kubainisha mipaka ili kupunguza migogoro
Ruvuga akiwaeleza wabunge mikakati mbalimbali ya kuboresha kilimo na masoko
Sophu akiwapongeza wabunge kushiriki kwenye mdahalo huo
Nsanzugwako akielezea kwa ufupi watakayoyafanya na Mviwata
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mviwata
Ruvuga akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philip Mulugo baada ya mdahalo kumalizika
No comments:
Post a Comment