Friday, June 17, 2016

KAMPUNI YA TING YATOA MAGETI YA CHUMA KUDHIBITI WEZI WA KOKI ZA MAJI UWANJA WA TAIFA


Naibu Waziri wa Habari, Uramaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura (wane kushoto), akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ting, Father Fernandez, wakati akipokea msaada wa mageti kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Juni 17, 2016. Kampuni hiyoimetoa mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44.


NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
KAMPUNI YA kusambaza ving'amuzi vya televisheni ya Ting ya jijini Darves Salaam, imekabidhi mageti ya chuma  27 kwa uongozi wa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ili kuwadhibiti “wakora” wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki za maji.
Akipokea msaada huo leo Juni 17, 2016 kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanjanin hapo, Naibu Waziri wa Habri, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura, ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo ambao utakomesha vitendo vya wizi na uharibifu wa miundo mbinu ya uwanja huo wa soka wa kisasa kabisa hapa nchini
“Mwanzoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu, nilifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huu na kujionea uharibifu mkubwa kwenye vyoo ambapo koki za maji zimeibiwa na hivyo kusababisha baadhi ya vyoo kufungwa na kupelekea usumbufu mkubwa kwa mashambiki was ok.” Alisema Naibu waziri.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ting, Mchungungaji Dkt. Veron Fernandos, alisema kampuni yake ambayo inajishughulisha na uagizaji na usambazaji wa ving’amuzi, imeona inao wajibu mkubwa wa kusaidia sekta ya michezo kwenye eneo hilo la kutunza miundombinu ya uwanja wa Taifa.
Alisema, Ting imetoa jumla ya mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44 ambayo yatasaidia kudhibiti wezi wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki na kuharibu miundombinu mingine.
K-VIS MEDIA imeshuhudia koki za maji kwenye baadhi ya vyoo zikiwa zimeng’olewa.

 Mkurugenzi wa kampuni ya Ting, Mchungaji Dkt. Vernon Fernados, akimuonyesha moja ya mageti hayo Naibu Waziri Anastazia James Wambura
 Mkazi wa jijini Dar es Salaam, akitoka kwenye vyoo vya juu vya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambavyo vimeathirika sana na wizi huo. Mageti hayo yatafungwa kwenye vyoo hivyo vya juu uwanja mzima
 Mkazi wa jiji akijisaidia kwenye moja ya vyoo hivo huku upande wa kushoto bomba linaonekana likiwa limeng'olewa koki
 Naibu Waziri akizungumza wakati wa makabidhiano hayo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Nkenyenge
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Nkenyenge, (kushoto), akizungumza mbele ya Naibu Waziri, Wambura (katikati) na Mkurugenzi wa Ting, Dkt. Fernados
 Naibu Waziri akizungumza na Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa, Julius Mgaya, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo
 Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa, Julius Mgaya, (katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ting, Dkt. Fernandos, wakimpokea Naibu Waziri
 Naibu Waziri akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ting, Dkt. Fernandos, wakati akiwasili uwanja wa Taifa kupokea mageti hayo
 Sehemu ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambao baadhi ya watu wamekuwa wakihujumu miundombinu yake
 Wafanyakazi wa kampuni ya Ting
 Mkurugenzi Mtendajiw a Kampuni ya Ting, akiwa na baadhi wa wafanyakazi na wawakilishi wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara
Nyasi za uwanja wa Taifa zikipunguzwa kwa mashine maalum

No comments: