WANAFUNZI wa chuo cha kodi(TRA) waaswa kutoa elimu ya maswala mbalimbali ya kodi kwa vijana wenzao ili kujifunza na kukuza uelewa wa kulipa kodi kwa hiyari.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa vijana wapewe elimu ya kulipa kodi kwa hiyari mapema ili kipindi watakapoanza kupata mapato waweze kulipa kodi bila kushurtishwa.
Amesema kuwa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni iliyofunguliwa leo iwe taa kwa jamii nzima na wanachama wa jumuiya hiyo waweze kutoa elimu ya kodi watakayoipata kwa wenzao ndani na nje ya mazingira ya chuo.
Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa huduma za wanafunzi wa chuo cha kodi- ITA, Rashid Mzava akizungumza na wanafunzi wa chuo cha kodi jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi.
Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Kodi(TRA)-ITA, Juma Nadhiru (Aliyesimamama) akizungumza na wanafunzi wa chuo cha kodi wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo, Pia amemshukuru mgeni rasmi kwa kufika katika chuo chao na kuwahamasisha wanafunzi wa chuo hicho kujifunza zaidi katika kuhamasisha jamii kulipa kodi kwa hiyari. Kaliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa huduma za wanafunzi wa chuo cha kodi- ITA, Rashid Mzava, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo , Meneja huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Honesta Ndunguru na Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Julieth Shehiza.
Kutoka kushoto ni Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Kodi(TRA)-ITA, Juma Nadhiru, Mkuu wa huduma za wanafunzi wa chuo cha kodi- ITA, Rashid Mzava, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo , Meneja huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Honesta Ndunguru na Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Julieth Shehiza wakiwa katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam.
Afisa Mahusiano wa chuo cha kodi (TRA), Rachel Mkundai akiwakaribisha na kuwatambulisha wageni waalikwa katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wa chuo cha kodi(TRA) wakiwa katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo.
Mwanafunzi wa chuo cha kodi (TRA), Busenene Malkia akichangia maada mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo.
2 comments:
safi sanaaaaaaaaaa kwa support yenu michuuzzzzzzzzzz
Ts the great move for all ITA's member under the leadership of "Be part of it,make it happen" of Mr.President of ITA,Juma Nadhiru.Hope to see alot of best to come.
By.Wise Man
Post a Comment